[ad_1]
Christian Eriksen aitwa kambini mwa Denmark kwa mara ya kwanza tangu Juni 2021
Na MASHIRIKA
CHRISTIAN Eriksen amejumuishwa katika kikosi cha Denmark kwa mara ya kwanza tangu apate matatizo ya moyo akichezea taifa lake kwenye fainali za Euro 2020 mnamo Juni 2021.
Kiungo huyo mbunifu mwenye umri wa miaka 30 aliwekewa kifaa maalum cha kumsaidia kudhibiti mapigo ya moyo tangu aanguke na kuzimia ghafla uwanjani akiwakilisha taifa lake dhidi ya Finland.
Mchezaji huyo wa zamani wa Tottenham Hotspur aliachiliwa na Inter Milan ya Italia baada ya tukio hilo na akasajiliwa na Brentford mnamo Januari 2022.
Denmark wameratibiwa kucheza dhidi ya Uholanzi kirafiki mnamo Machi 26 kabla ya kumenyana na Serbia mnamo Machi 29, 2022.
Eriksen ataungana na wachezaji wenzake wa Denmark nchini Uhispania kwa mazoezi zaidi kabla ya kutandazwa kwa mechi hizo mbili za kupimana nguvu.
Alijiunga na Brentford kwa mkataba wa miezi sita na akawajibishwa kwa mara ya kwanza katika mchuano uliomshuhudia akitokea benchi dhidi ya Newcastle United mnamo Februari 26, 2022.
TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO
[ad_2]
Source link