Askofu wa Kanisa la Anglikana dayosisi ya Malindi awataka viongozi wa dini wajitenge na siasa za migawanyiko
NA MAUREEN ONGALA
ASKOFU mkuu wa Kanisa la Angilikana Dayosisi ya Malindi, Ruben Katite amewashauri viongozi wa dini ya Kikristo wajitenge na siasa zinazoweza kuchagia migawanyiko katika jamii.
Aidha, alisema waumini hawafai kubaguliwa na kanisa kwa sababu tu ya miegemeo yao ya kisiasa kama watu binafsi wenye uhuru wa kujichagulia viongozi wanaowataka.
Pia amewataka vijana kutotumika vibaya na wanasiasa wakati huu wa siasa motomoto.