Connect with us

General News

Sabina Chege asema Karua ana ushawishi wa kuvutia kura nyingi kwa Azimio – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Sabina Chege asema Karua ana ushawishi wa kuvutia kura nyingi kwa Azimio – Taifa Leo

Sabina Chege asema Karua ana ushawishi wa kuvutia kura nyingi kwa Azimio

NA WACHIRA ELISHAPAN

UAMUZI wa kinara wa Narc-Kenya Bi Martha Karua kujiunga na vuguvugu la Azimio la Umoja umepokelewa kwa mbwembwe na viongozi wa mrengo wa Kinara Wa ODM Raila Odinga.

Kati ya walioridhika na uamuzi huo ni Mbunge Mwakilishi wa Kike katika Kaunti ya Muranga Bi Sabina Chege ambaye alimsifu Bi Karua akisema kwamba usemi mkubwa wa Bi Karua una uwezo wa kusawazisha hesabu ya kura za vuguvugu la Azimio katika uchaguzi mkuu wa Agosti iwapo atafanikiwa kutwaa nafasi ya Unaibu wa Rais.

Semi za Bi Chege zimejiri muda mfupi tu baada ya Bi Karua kutangaza kumuunga mkono Bw Odinga katika azma yake ya kuwania urais.

Msimamizi huyu wa wanawake, alisema kwamba hatua ya Bi Karua kujiunga na Azimio la Umoja itasaidia kuongeza kura za vuguzugu la Azimio huku siasa za Bw Odinga zikipigwa jeki pakubwa.

Aidha akizungumza na kituo cha Runinga cha Citizen, Bi Chege alisema kwamba usemi wa Bi Karua usioteteleka kisiasa ni ishara kwamba atawawezesha wengi kukata kauli kujiunga na kambi ya Bw Odinga.

“Ni habari njema kote nchini. Kwa chama kitakachomteua mwanamke kuwa Naibu wake, nina uhakika sasa wanawake wote watapiga kura kwa chama kama hicho. Naona sasa hata wanawake wanaopania kutafuta nyadhifa za uongozi wamepata kielelezo kutoka kwa Karua, alisema Bi Chege.

Kadhalika alimtaja Bi Karua kama mmoja wa waliofuzu kuwa kinara mwenza wa Bw Odinga anapokabiliana na Naibu wa Rais William Ruto ambaye anawania Urais kwa tiketi ya chama cha UDA.

“Karua ana tajriba pana na mwenye sifa za uongozi na mimi siwezi kusema kwamba hafai wadhifa wa kinara mwenza kwa Bw Odinga. Amekuwa katika serikali na anajua jinsi shughuli za serikali huendeshwa, kama zile enzi za Hayati Mzee Moi na Rais Mstaafu Mwai Kibaki,”akasema mwanahabari huyu wa zamani.

Hata hivyo Mbunge Mwakilishi wa Kike katika Kaunti ya Uasin Gishu Gladys Shollei ametupilia mbali uwezekano wa Bi Karua kutwaa nafasi ya Kinara mwenza wa Azimio la Umoja akisema kwamba chama cha ODM na Azimio havina wanawake wengi na kwamba chama hicho cha ODM kilimkabidhi Mbunge Mwakilishi wa Kike katika Kaunti ya Homabay Bi Gladys Wanga wadhifa wa kamati ya Bunge kuhusu Fedha, baada ya handisheki kati ya Rais Uhuru Kenyatta na kinara wa ODM Raila Odinga, mapema mwaka wa 2018 na wala si kabla ya hapo.

“Ningefurahia sana iwapo Azimio ingemteua kinara mwenza mwanamke, hasa ikiwa ni Martha Karua, lakini tunajua ODM haijawahi kuwa na viongozi wanawake hata katika Bunge. Viongozi wote ni wanaume isipokuwa Dkt Sally Kosgei ambaye kwa sasa yuko kwenye kampeni za Bw Odinga. Mengi hivyo basi yafaa kufanywa katika kambi ya Odinga,”alisema Bi Gladys Shollei.

Sasa huenda uamuzi wa Bi Karua ukavutia wanawake wengi nchini katika kuwania nyadhifa za juu zaidi, hali ambayo bila shaka itabadilisha mkondo wa siasa za Kenya.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending