Connect with us

General News

Mwanafunzi hutii mno sheria anapohusishwa vyema katika kuibuni – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mwanafunzi hutii mno sheria anapohusishwa vyema katika kuibuni – Taifa Leo

CHAKULA CHA UBONGO: Mwanafunzi hutii mno sheria anapohusishwa vyema katika kuibuni

VIJANA ambao ndio asilimia kubwa ya wanafunzi, ni miongoni mwa wanajamii wanaowania uhuru wao mno.

Hata pale ambapo sheria zilizopo ni kwa faida yao, hutaka wajiamulie mambo. Suala hili huchangiwa zaidi na ukweli kwamba vijana wanapobaleghe au kuvunja ungo huwa miongoni mwa watu wa kipekee katika jamii.

Mihemko yao hubadilika na kuwaweka katika ngazi tofauti na wanajamii wengine. Ukumbuke pia kwamba hiki ndicho kipindi chao cha ujitambuaji; hivyo, hufanya mambo mengine kama majaribio waone yatakayojiri. Wanaamini kila mmoja aliyepitia umri huo alipewa uhuru wake, mbona wao wanyimwe?

Matazamio haya ya kijana yana mashiko kwa kiasi fulani. Kwa kweli, hapaswi kunyimwa kabisa uhuru wa kujiamulia bali ahitaji sana kuelekezwa kuhusu uhuru huo.

Mathalan, anapotaka kulala kwa zaidi ya muda unaoendana na umri wake, ahitaji kukumbushwa kwamba uvivu wake unaambatana na gharama fulani.

Akifanya udanganyifu katika mitihani, dhaifu zake halisi hazitagunduliwa na hivyo hatapata maelekezo na nasaha mwafaka kuhusu taaluma ya kujiunga nayo.

Kwa hivyo ni lipi linalopasa kufanywa? Lifanywe vipi? Hatua mwafaka ya kuchukua ni kumjumuisha mwanafunzi katika kubuni kanuni na sheria zinazomhusu.

Mwombe ajiwazie kama mzazi, mwalimu, mfadhili, mwangalizi. Je katika nafasi hiyo angependa wanawe au wategemezi wake wawajibike vipi? Je, anaweza kuwapa uhuru kiasi gani?

Mwelekeze apendekeze matukio atakayoyachukulia kuwa makosa na apendekeze adhabu mwafaka kwa kila mojawapo.

Katika harakati hiyo anaweza kupindapinda kidogo lakini hatimaye zoezi hili litamkomaza.

Ingawa hatakiri hivyo, atakapopata fursa ya kuyawazia mwenyewe, aweza kujirudi kidogo. Mkumbushe pia kuwa mustakabali wake unategemea hatua azichukuazo sasa; kuziwajibikia ni jambo la umuhimu mkubwa.