Connect with us

General News

Achani aponda wapinzani kuhusu maendeleo Kwale – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Achani aponda wapinzani kuhusu maendeleo Kwale – Taifa Leo

Achani aponda wapinzani kuhusu maendeleo Kwale

NA KNA

NAIBU Gavana wa Kwale, Bi Fatuma Achani, ametoa changamoto kwa wapinzani wake katika kinyang’anyiro cha ugavana, waeleze wananchi maendeleo ambayo wamewaletea kufika sasa.

Akizungumza wakati wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa zahanati ya Galana na bweni la chuo anwai cha Galana, katika Wadi ya Tsimba/Golini, Kaunti Ndogo ya Matuga, Bi Achani alidai kuwa, tofauti na wenzake, yeye tayari ameonyesha uwezo wake wa kubadili maisha ya wananchi.

“Niko tayari zaidi na nimepata ujuzi wa kutosha kuongoza na nishaonyesha haya kupitia kwa miradi ya kubadili maisha ambayo tulianzisha kwa miaka kumi iliyopita. Wapinzani wangu hawana chochote cha kuonyesha kwa hivyo nawaomba wapigakura wanichague ifikapo Agosti 9,” akasema.

Akiwa ameandamana na Gavana Salim Mvurya, naibu gavana huyo ambaye amepanga kuwania ugavana kupitia Chama cha UDA, alimpigia debe Naibu Rais William Ruto kurithi kiti cha Rais Uhuru Kenyatta.

Bw Mvurya, anayetumikia kipindi chake cha pili, aliwataka wanasiasa kutotumia suala la jinsia kumpinga naibu wake.

“Wanawake ni viongozi bora wanaostahili heshima. Achani amehitimu kuchukua nafasi hii kutoka kwangu ili awe gavana wa kwanza wa kike katika eneo la Pwani,” akasema.

Kinyang’anyiro cha kurithi kiti cha Bw Mvurya, kimevutia wagombeaji wengi akiwemo waziri wa zamani, Bw Chirau Mwakwere, aliyekuwa katibu wa wizara ya kilimo, Prof Hamadi Boga, Spika wa Bunge la Kaunti, Bw Sammy Ruwa, Seneta Maalumu wa ODM, Dkt Agnes Zani, aliyekuwa mhandisi katika Bandari ya Mombasa, Bw Chai Lung’anzi, mfanyabiashara, Bw Daniel Dena na Bw Suleiman Lugogo.

Bi Achani alimtangaza Diwani wa Wadi ya Samburu/Chengoni, Bw Josephat Chirema Kombo, awe mgombea mwenza wake, huku Prof Boga akimtangaza katibu wa wizara ya utalii, Bi Safina Kwekwe kwa nafasi hiyo.

Katika kampeni zake, Prof Boga ambaye anataka kushindania tikiti ya Chama cha ODM, husisitiza kuhusu hitaji la kubadili mbinu za kilimo Kwale huku akisema hilo litakuwa jukumu lake kuu endapo atashinda ugavana.

Kulingana naye, uzalishaji chakula utazidishwa tu iwapo wakulima wadogo katika eneo hilo watapewa uwezo kupitia kwa utumizi wa mbinu za kisasa za kilimo na kuongeza ubora wa mazao yao.

“Mtu yeyote anayetaka kuongoza Kwale lazima awe na mpango maalumu utakaolenga kuwezesha wakulima. Kustawisha kilimo kutasaidia kuongeza viwango vya mazao, kutoa nafasi ya ajira kwa vijana na pia kukabiliana na njaa,” akasema akiwa katika kampeni Kaunti Ndogo ya Msambweni.

Prof Boga aliahidi kujenga vituo vya kilimo biashara katika kila kaunti ndogo ya Kwale ili kustawisha kilimo iwapo atachaguliwa kuwa gavana katika uchaguzi ujao.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending