[ad_1]
Mwaniaji urais sasa ahamia ELP kutoka Ford Asili
NA WINNIE ONYANDO
MFANYABISHARA Grita Muthoni, amejiondoa katika chama cha Ford Asili na kujiunga na chama cha Empowerment and Liberation Party (ELP) baada ya kukataliwa hadharani na katibu wa chama hicho.
Akizungumza na wanahabari jana jijini Nairobi, Bi Muthoni alisema kuwa atapeperusha bendera ya urais kupitia chama hicho.Alishutumu hatua ya kukataliwa na Njeru Kathangu kuwa yeye si mwanachama wa Ford Asili.
“Sikufurahia kilichotokea nilipokuwa nikihojiwa katika televisheni ya Citizen. Bw Kathangu alisema hadharani kuwa mimi si mwanachama wa Ford Asili. Hata hivyo, namshukuru kiongozi wa chama cha ELP, Rose Mulwa, kwa kunikaribisha katika chama chake,” akasema Bi Muthoni.
[ad_2]
Source link