Connect with us

General News

Waliojaribu kuiba mtihani kuadhibiwa – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Waliojaribu kuiba mtihani kuadhibiwa – Taifa Leo

#KCPE2021: Waliojaribu kuiba mtihani kuadhibiwa

Na CHARLES WASONGA

WAZIRI wa Elimu, Prof George Magoha ameshikilia kuwa hapakuwa na visa vya wizi katika mtihani wa kitaifa wa darasa la nane (KCPE) aliyotangaza matokeo yake Jumatatu.

Hata hivyo, alisema kwamba watahiniwa 320 walijaribu kushirikiana na maafisa wa kusimamia mitihani na walimu ili kudanganya na kwamba wataadhibiwa.

Akiongea katika makao makuu ya baraza la mitihani nchini (KNEC) jijini Nairobi, Prof Magoha, hata hivyo, alisema baadhi ya walimu walijaribu kupiga picha karatasi za mitihani, “japo baada ya watahiniwa kuangia ndani ya madarasa.”

“Maafisa wetu wa usalama kwa ushirikiano na wenzao kutoka asasi nyingine za serikali walikuwa macho kuziba mianya yoyote ambayo ingefanikisha wizi wa mtihani huo,” Prof Magoha alisema.

“Kwa hivyo, ningependa kuwahakikishia kuwa mtihani huu haukuibiwa. Kwa hivyo, wanahabari hawana cha kuandika,” akaongeza.

Prof Magoha alisema wakati wa kusahihishwa kwa mtihani huo, KNEC iligundua kuwa watahiniwa 320 katika vituo saba walishirikiana wakifanya mtihani huo wa KCPE wa 2021. “Watahiniwa hawa hawajapewa alama katika masomo husika,” Waziri akaeleza.

Hii ina maana kuwa huenda watahiniwa kama hao hawatapata matokeo yao na hivyo huenda wakakosa kujiunga na shule za upili, pamoja na wenzao, kuanzia Mei mwaka huu.

Jumla ya watahiniwa 1,214, 031 walifanya mtihani huo mapema mwezi huu wa Machi katika vituo 28,313 kote nchini.Waziri Magoha alisema wale wote ambao watapata matokeo yao wataweza kujiunga na shule za upili.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending