Connect with us

General News

Msichana wa pili bora nchini afichua ndoto yake ya kuwa wakili wa kimataifa – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Msichana wa pili bora nchini afichua ndoto yake ya kuwa wakili wa kimataifa – Taifa Leo

KCPE 2021: Msichana wa pili bora nchini afichua ndoto yake ya kuwa wakili wa kimataifa

NA MWANGI MUIRURI

MBUGUA Sharon Wairimu Muteti, 14, aliyeibuka msichana wa pili bora akiwa na alama 426 amesema anataka awe wakili.

Amesema kwamba angependelea kuwa wakili wa masuala ya haki za binadamu haswa za wanawake.

Sharon alifanyia mtihani wake katika Shule ya Msingi ya Emmanuel iliyoko katika mji wa Kangari, Kaunti ya Murang’a.

Alisema Jumatatu kwamba lengo lake sasa ni kujiunga na Shule ya Upili ya Wasichana ya Alliance na hatimaye ahitimu kujiunga na chuo kikuu.

“Ndio tena nisake mwanya wa kuimarika kitaaluma katika fani ya uanasheria Mungu akinijalia, nifuatane na utaalamu katika safu ya ulimwengu,” akasema.

Shule ya kina Sharon ilisajili watahiniwa 117 na ambapo 60 kati yao walipata alama 400 kwenda juu.

Shule yenyewe ilipata alama wastani 400.52 kumaanisha kwa kweli watahiniwa wake walifanya vyema.

Mamake Sharon, Bi Serah Watiri alimtaja kuwa mwenye bidii ya mchwa, mwadilifu, mcha Mungu na mwenye heshima.

Mwalimu mkuu katika wa Shule hiyo ya Emmanuel Bw Muriithi Thiaka alisema wadau wote wanamshukuru Maulana kwa ufanisi huo na pia akaipa kongole Wizara ya Elimu kwa jinsi ilivyoandaa mtihani huo.