[ad_1]
Mvutano wa Sossion, KNUT waelekezwa kwa uteuzi wa UDA Bomet
NA VITALIS KIMUTAI
MVUTANO unaoendelea kati ya mbunge maalum wa Orange Democratic Movement (ODM), Wilson Sossion na maafisa wa Chama cha Kitaifa cha Walimu (KNUT), wakiongozwa na Katibu Mkuu Collins Oyuu, umeenea hadi kwenye kampeni za kugombea useneta Kaunti ya Bomet.
Hatua hiyo imepandisha joto la kisiasa eneo hilo, wiki mbili kabla ya chaguzi za mchujo za United Democratic Alliance (UDA, zinazotarajiwa kuwa na ushindani mkali.
Maafisa wa KNUT wametangaza wazi kumuunga mkono wakili wa Nairobi, Bw Hillary Sigei, ambaye pamoja na Bw Sossion na Seneta anayeongoza kwa sasa Dkt Christopher Langat, wanashindania tiketi ya UDA kuhusiana na kiti hicho cha useneta katika teuzi za mchujo zitakazofanyika Aprili 14.
Bw Sigei ambaye ni wakili wa chama cha UDA, ni mwandani wa karibu wa Naibu Rais William Ruto na mshirika katika kampuni ya huduma za kisheria lililopo Nairobi la Singoei, Murkomen na Sigei.
“Tunamuunga mkono Bw Sigei ambaye ni wakili wa KNUT na tuna imani katika uongozi wake. Tunawahimiza wapiga kura Kaunti ya Bomet kumpigia debe kwa wadhifa wa useneta katika teuzi za mchujo na uchaguzi mkuu wa Agosti 9,” alisema Bw Mutai, afisa mkuu wa KNUT katika eneo la Bonde la Ufa.
Next article
Wetang’ula asuta Raila kuhusu ahadi za kufufua viwanda…
[ad_2]
Source link