Connect with us

General News

Mbappe ang’aa PSG ikiponda Lorient ligini – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mbappe ang’aa PSG ikiponda Lorient ligini – Taifa Leo

Mbappe ang’aa PSG ikiponda Lorient ligini

Na MASHIRIKA

KYLIAN Mbappe alifunga mabao mawili na kuchangia matatu mengine katika ushindi wa 5-1 uliosajiliwa na Paris Saint-Germain (PSG) dhidi ya Lorient katika Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1).

Neymar alifungulia PSG ukurasa wa mabao katika dakika ya 12 kabla ya kufungia miamba hao goli la tano kunako dakika ya 90. Magoli yote hayo yalichangiwa na Mbappe ambaye sasa anajivunia mabao 17 katika Ligue 1 msimu huu.

Mbappe alipachika wavuni mabao yake katika dakika za 28 na 67 kabla ya kutoa krosi iliyojazwa kimiani na Lionel Messi katika dakika ya 73.

Terem Moffi alifutia Lorient machozi katika dakika ya 56. PSG sasa wanaselelea kileleni mwa jedwali la Ligue 1 kwa alama 68 huku pengo la pointi 12 likitamalaki kati yao na nambari mbili Olympique Marseille waliotandika Saint-Etienne 4-2. Mabingwa watetezi Lille wanashikilia nafasi ya saba kwa alama 47 sawa na namabari sita AS Monaco waliocharaza Metz 2-1.

MATOKEO YA LIGUE 1 (Aprili 3, 2022):

PSG 5-1 Lorient

Strasbourg 1-0 Lens

Clermont 2-3 Nantes

Metz 1-2 Monaco

Montpellier 1-2 Brest

St-Etienne 2-4 Marseille

Troyes 1-0 Reims

Lyon 3-2 Angers

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending