Connect with us

General News

Baraza Kuu la ODM sasa laingilia kati mzozo kuhusu mchujo Kaunti ya Mombasa – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Baraza Kuu la ODM sasa laingilia kati mzozo kuhusu mchujo Kaunti ya Mombasa – Taifa Leo

Baraza Kuu la ODM sasa laingilia kati mzozo kuhusu mchujo Kaunti ya Mombasa

NA SAMWEL OWINO

BARAZA Kuu la Chama cha ODM limeingilia kati mzozo kuhusu mbinu ya kuchagua wagombeaji wa viti mbalimbali katika Kaunti ya Mombasa.

Baraza hilo ni la pili kwa ukuu wa madaraka ya ODM.

Mkutano wa leo Jumanne uliitishwa baada ya malalamishi kuibuka kuhusu uwezekano wa baadhi ya wagombeaji kupewa tikiti za moja kwa moja.

Mbunge wa Mvita, Bw Abdulswamad Nassir, ni miongoni mwa wale waliotarajiwa kupewa tikiti baada ya kura za maoni zilizodhaminiwa na ODM kuonyesha ana umaarufu kumliko mpinzani wake wa karibu, Bw Suleiman Shahbal.

Wengine waliotarajiwa kupewa tikiti ni Mbunge wa Changamwe, Bw Omar Mwinyi, aliyekuwa Mbunge wa Kisauni, Bw Rashid Bedzimba, Seneta Mohamed Faki na Bw Said Abdalla almaarufu kama Saido anayetaka kuwania ubunge Nyali.

Mwenyekiti wa ODM, Bw John Mbadi, alithibitisha jana Jumatatu majina hayo yaliorodheshwa miongoni mwa wanaozingatiwa kwa sababu ya umaarufu wao, lakini hakuna aliyepewa tikiti.

Kulingana naye, mkutano umeitishwa leo Jumanne kwa vile matokeo ya kura za maoni yalipingwa na wengine.

“Nia ya chama ni kwamba, kabla kumkabidhi mtu tikiti, lazima kuwe na maelewano baina ya wagombeaji. Hatupeani tu tikiti ovyo. Lakini mkutano wetu wa Alhamisi iliyopita haukufanikiwa kuzaa makubaliano kwa hivyo uamuzi haujafanywa kuhusu suala hilo,” akasema.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending