Connect with us

General News

Raila hajafika katika afisi za NCIC kuhojiwa – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Raila hajafika katika afisi za NCIC kuhojiwa – Taifa Leo

TUSIJE TUKASAHAU: Raila hajafika katika afisi za NCIC kuhojiwa

MNAMO Machi 11, 2022 mwaniaji urais wa muungano wa Azimio One Kenya Raila Odinga aliagizwa kufika mbele ya Tume ya Kitaifa ya Uwiano na Utangamano (NCIC) kujibu kuhojiwa kwa kutumia neno “madoadoa” akiendesha kampeni kaunti ya Wajir.

Kwa kuwa Bw Odinga alikuwa nje ya nchi, mwenyekiti wa tume hiyo Dkt Samuel Kobia alisema kuwa Bw Odinga angefika mbele ya maafisa wake kuelezea madai hayo baada ya kuwasili kutoka Uingereza.

Alisema afisi yake ilikuwa ikichunguza madai hayo.

Bw Odinga alirejea nchini mnamo Machi 22, 2022 baada ya kukamilisha ziara hiyo ya wiki moja. Lakini tangu wakati huo, mwanasiasa huyo hajafika katika afisi za NCIC kuhojiwa kuhusiasa na matamshi hayo yalifasiriwa kama uchochezi wa chuki.

Safu hii inaikumbusha NCIC, na mwenyekiti wake Dkt Kobia, kwamba isije ikasahau kutimiza ahadi yake ya kumdadisi Bw Odinga kuhusiana na matamshi.

Dkt Kobia akumbuke kuwa mnamo Januari 2022 tume yake ilikuwa mwepesi kumchukulia hatua Seneta wa Meru Mithika Linturi kwa kutumia neno lilo hilo la “madoadoa” katika mkutano wa kisiasa mjini Eldoret.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending