Connect with us

General News

Mswada unaolenga kupunguza ushuru kwa mafuta ungali umekwama bungeni – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mswada unaolenga kupunguza ushuru kwa mafuta ungali umekwama bungeni – Taifa Leo

TUSIJE TUKASAHAU: Mswada unaolenga kupunguza ushuru kwa mafuta ungali umekwama bungeni

MNAMO Jumatatu wiki hii serikali ilitenga Sh34 bilioni katika bajeti ya ziada ya Sh139 bilioni, pesa za kulipwa kampuni za mafuta kufidia hasara zinazopata kwa kuuza mafuta kwa bei zilizowekwa na Mamlaka ya Kusimamia Sekta ya Kawi na Mafuta (EPRA).

Hii ni baada ya taifa kukumbwa na uhaba wa mafuta kufuatia hatua ya kampuni hizo kuhodhi bidhaa hizo kuishinikiza serikali izilipe malimbikizi ya malipo ya tangu Septemba 2021.

Hata hivyo, Rais Uhuru Kenyatta, ambaye alitia saini mswada wa bajeti hiyo ya ziada, asisahau kuwa kando na kupanda kwa bei ya mafuta katika masoko ya nje, bidhaa hiyo ni ghali nchini kwa sababu ya ushuru mwingi unaotozwa na serikali yake.

Wataalamu wanakadiria kuwa karibu asilimia 50 ya bei ya aina zote za mafuta huchangiwa na aina mbalimbali za ushuru, ukiwemo ushuru wa thamani, (VAT).

Suluhu kwa tatizo hili iko katika mswada unaolenga kupunguza ushuru kwa mafuta na ambao umekwama bungeni licha ya kuwasilishwa na mwenyekiti wa Kamati ya Bunge kuhusu Fedha Gladys Wanga Novemba 30, 2021.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending