Connect with us

General News

Serikali ya Trans-Nzoia yalaumiwa kwa ukosefu wa dawa hospitalini – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Serikali ya Trans-Nzoia yalaumiwa kwa ukosefu wa dawa hospitalini – Taifa Leo

Serikali ya Trans-Nzoia yalaumiwa kwa ukosefu wa dawa hospitalini

NA GERALD BWISA

SERIKALI ya kaunti ya Trans-Nzoia inalaumiwa kwa ukosefu wa vifaa vya kimatibabu katika vituo vya afya katika kaunti hiyo.

Mnamo Jumanne wahudumu wa afya walifanya maandamano wakilalamikia hali hiyo ambayo imewaacha wagonjwa wakiteseka.

Kulingana na wahudumu hao, changamoto hiyo imedumu kwa muda wa miezi mitatu iliyopita na serikali hiyo inayoongozwa na Gavana Patrick Khaemba haijachukua hatua zozote kuimarisha hali.

Hospitali ya Rufaa ya Kitale ndio iliyoathirika zaidi licha ya kwamba ndio hupokea idadi kubwa ya wagonjwa.

Madaktari na wauguzi wanasema hospitali hiyo, sawa na zingine katika kaunti hiyo haina dawa na vifaa vingine vya kimatibabu.

Kando na vifaa vya afya, hospitali nyingi hazina vyakula vya kimsingi kama vile maziwa. Wagonjwa wanalazimika kunywa chai isiyo na maziwa.

Jumanne, wahudumu hao wa afya walipiga kambi katika afisi ya Gavana Khaemba wakitaka azungumze nao.

Aidha, waliapa kulemaza shughuli zote katika hospitali na vituo vingine vya afya ikiwa serikali hiyo hataishughulikia malalamishi yao.

Wagonjwa pia wamelalamika kuwa wanalazimishwa kununua dawa kutoka kwa maduka ya kibinafsi, wengi wakielezea kulemewe na gharama hiyo.

“Licha ya kuhakikishiwa kuwa kuna dawa katika hospitali za kaunti, hali ni tofauti kwamba kwa muda wa miezi sita, tumekuwa tukishauriwa k kununua dawa katika maduka fulani mjini Kitale. Hatuwezi kumuda gharama hii kwa sababu dawa zingine ni ghali mno,” James Wafula, ambaye ni mkazi wa Kitale alisema.