Connect with us

General News

Jinsi ya kuoka keki mchanganyiko wa unga – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

MAPISHI KIKWETU: Jinsi ya kuoka keki mchanganyiko wa unga

MAPISHI KIKWETU: Jinsi ya kuoka keki mchanganyiko wa unga

NA MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Dakika 20

Muda wa mapishi: Dakika 50

Walaji: 6

Vinavyohitajika

– ½ kikombe cha siagi

– kikombe 1 cha sukari

– mayai 2

– kijiko 1 cha maganda ya limau yaliyokunwa

– kikombe 1 unga wa ngano

– kikombe 1 cha unga wa mtama

– ½ ya kikombe cha wanga wa viazi

– vijiko 2 vikubwa vya unga wa muhogo

– kijiko ½ cha baking powder

– kijiko ½ baking soda

– chumvi kiasi cha ¼ kijiko cha chai

– ¾ kikombe cha maziwa

– kijiko kimoja cha chai cha vanilla

Maelekezo

Washa ovena na subiri joto lifikie nyuzijoto 160. Paka mafuta ya kutosha kwenye chombo cha kuokea keki. Viache vitulie.

Kwa kutumia miksa ya umeme na bakuli kubwa la kuchanganyia, changanya siagi, sukari na mayai kwa kasi ya kiwango wastani hadi vichanganyike vizuri.

Ongeza maganda ya limau.

Katika bakuli la ukubwa wa kati, changanya unga wa ngano, “baking powder”, “baking soda”, na chumvi.

Changanya maziwa na vanilla katika kikombe cha kupimia.

Kwa kutumia miksa katika kasi ya chini, changanya viungo vikavu kwenye mchanganyiko wa mayai, ukibadilishana na maziwa.

Ukianzia na kumalizia na viungo vikavu. Changanya hadi vichanganyike sawa sawa. Kwa kutumia kijiko, weka siagi kwenye chmbo cha kuokea.

Oka keki kwa muda wa dakika 50 kutegemea ukubwa wa kikaangio, au hadi sehemu ya juu ya keki iwe rangi ya kahawia iliyoiva.

Iache keki ipoe kwa dakika 5 kisha itoe kwenye kikaango na iache ipoe vizuri.

Ikate keki na ufurahie.