Connect with us

General News

Magoha atetea mgao mkubwa kwa maskini – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Magoha atetea mgao mkubwa kwa maskini – Taifa Leo

Magoha atetea mgao mkubwa kwa maskini

Na KENYA NEWS AGENCY

WAZIRI wa Elimu Prof George Magoha ametetea hatua ya serikali kutengea kiasi kikubwa cha hazina ya makundi yaliyotengwa kwa wanafunzi wanaotoka kwenye mitaa ya mabanda.

Prof Magoha alisema wanafunzi hao wanastahili kupata elimu bora licha ya umaskini mkubwa ambao wanakumbana nao katika mitaa hiyo ya mabanda.

“Watoto kutoka mtaa wa mabanda wa Kiandutu, Thika na Mji wa Huruma, Nairobi walipewa pesa za kujiunga na vyuo vikuu. Lazima tuhakikishe kuwa hata maslahi ya wale ambao wamelemewa na umaskini yanatiliwa manani,” akasema.

Alikuwa akizungumza baada ya kuzindua ujenzi wa madarasa ya CBC katika Shule ya Upili ya Muchungucha, Murang’a ambapo alihakikishia wanafunzi kutoka jamii maskini nafasi ya kujiunga na vyuo vikuu cha kitaifa.

Prof Magoha aliongeza kuwa, yeye binafsi alinufaikia na mpango wa ufadhili uliokuwa ukiendeshwa na wakfu wa Jomo Kenyatta. Aidha, aliwataka Wakenya wenye mapato ya kadri ambao wana uwezo wa kuwapeleka watoto wao katika shule za kibinafsi, wafanye hivyo ili kupunguza msongamano katika shule za umma na pia kuwapa wanafunzi kutoka jamii maskini nafasi ya kuendeleza masomo.