Connect with us

General News

Tulifanya kila liwezekanalo kumshawishi kocha Erik ten Hag asalie kambini mwetu – Ajax – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Tulifanya kila liwezekanalo kumshawishi kocha Erik ten Hag asalie kambini mwetu – Ajax – Taifa Leo

Tulifanya kila liwezekanalo kumshawishi kocha Erik ten Hag asalie kambini mwetu – Ajax

Na MASHIRIKA

MKURUGENZI wa kiufundi kambini mwa Ajax, Gerry Hamstra amesema usimamizi wa kikosi hicho ulifanya kila liwezekanalo kumdumisha kocha Erik ten Hag kambini mwao.

Manchester United wako pua na mdomo kumpokeza mkufunzi huyo mikoba yao kwa mkataba wa miaka mitatu katika hatua ya kujaza pengo la Ole Gunnar Solskjaer aliyetimuliwa Novemba 2021 kutokana na matokeo duni. Mikoba ya mabingwa hao mara 20 wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) sasa inashikiliwa na mkufunzi Ralf Rangnick.

Ajax walipigwa na PSV Eindhoven 2-1 katika fainali ya Dutch Cup mnamo Aprili 17, 2022 na walidenguliwa na Benfica ya Ureno katika hatua ya 16-bora kwenye kampeni za Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) msimu huu.

“Tunatarajia asalie nasi licha ya hatua iliyopigwa na Man-United katika mchakato wa kumsajili. Bado hajaagana nasi wala kutufahamisha kuhusu maagano aliyo nayo na Man-United,” akasema Hamstra.

Ten Hag hakutarajiwa kuthibitishwa kuwa kocha mpya wa Man-United kabla ya fainali ya Dutch Cup kusakatwa.

Kufikia sasa, Ajax wanadhibiti kileleni cha jedwali la Ligi Kuu ya Uholanzi (Eredivisie) kwa alama nne zaidi kuliko nambari mbili PSV. Ajax wanapigiwa upatu wa kunyanyua ubingwa wa Eredivisie kwa mara ya tatu chini ya Ten Hag.

Kwa mujibu wa magazeti mengi nchini Uingereza, Ten Hag, 52, ataanza kunoa kikosi cha Man-United mwishoni mwa msimu huu. Atakuwa radhi kurefusha kandarasi yake uwanjani Old Trafford kwa mwaka mmoja zaidi kutegemea matokeo ya Man-United chini ya ukufunzi wake.

Kocha wa zamani wa Tottenham Hotspur ambaye sasa anadhibiti mikoba ya Paris St-Germain (PSG) ya Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1), Mauricio Pochettino alikuwa pia akipigiwa upatu wa kupokezwa mikoba ya Man-United.

Kibarua kigumu zaidi kwa Ten Hag ni kushughulikia mustakabali wa kitaaluma wa wanasoka Paul Pogba, Jesse Lingard, Cristiano Ronaldo na Marcus Rashford wanaohusishwa na uwezekano mkubwa wa kuondoka Old Trafford mwishoni mwa muhula huu.

Ten Hag atakuwa kocha wa tano baada ya David Moyes, Louis van Gaal, Jose Mourinho na Solskjaer kupokezwa wa mkataba wa kudumu kambini mwa Man-United tangu mkufunzi Sir Alex Ferguson astaafu mnamo 2013.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending