Connect with us

General News

Kalonzo akome kuyumba, afanye maamuzi mwafaka sasa ili ajinusuru kisiasa – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Kalonzo akome kuyumba, afanye maamuzi mwafaka sasa ili ajinusuru kisiasa – Taifa Leo

WANDERI KAMAU: Kalonzo akome kuyumba, afanye maamuzi mwafaka sasa ili ajinusuru kisiasa

NA WANDERI KAMAU

KIONGOZI wa Wiper, Bw Kalonzo Musyoka, ni miongoni mwa wanasiasa wenye tajriba kubwa zaidi ya kisiasa nchini.

Amekuwa siasani kwa zaidi ya miongo mitatu, tangu alipochaguliwa kama mbunge wa Kitui Kaskazini mnamo 1985.

Amehudumu katika serikali za marehemu Daniel Moi na Rais Mstaafu Mwai Kibaki—kama waziri na Makamu wa Rais mtawalia.

Vile vile, amehudumu katika serikali ya Rais Uhuru Kenyatta kama Mjumbe Maalum wa Kenya nchini Sudan Kusini, kuyapatanisha makundi mbalimbali yanayozozana.

Hivyo, amehudumu katika serikali za marais watatu.Hiyo ni tajriba pana ya kisiasa inayofaa kumsaidia Bw Musyoka kuusoma na kuuelewa mwelekeo wa kisiasa nchini.

Hata hivyo, inasikitisha kuwa hadi sasa, Bw Musyoka bado anayumba kuhusu ni mwelekeo upi wa kisiasa anaofaa kufuata, uchaguzi mkuu wa Agosti unapoendelea kukaribia.

Ingawa yupo katika mrengo wa Azimio la Umoja-One Kenya unaoongozwa na kiongozi wa ODM, Bw Raila Odinga, Bw Musyoka anaonyesha dalili za mpenzi aliye katika uhusiano ambao haumridhishi hata kidogo.

Tangu kujiunga na mrengo huo, Bw Musyoka na washirika wake wamekuwa wakitoa msururu wa malalamishi ya “kutojumuishwa ifaavyo” kwenye mrengo huo, hali inayotajwa kumkasirisha Rais Kenyatta.

Washirika wake wa karibu kama Seneta Mutula Kilonzo Junior (Makueni) na Enoch Wambua (Kitui) wamekuwa wakitishia kwamba huenda Bw Musyoka akajitoa kwenye mrengo huo ikiwa hatafanywa kuwa mgombea-mwenza wa Bw Odinga.

Matakwa hayo ya Bw Musyoka yanaonekana kuwa mwanzo mbaya kwa Azimio, ikizingatiwa kuwa uthabiti wa kisiasa wa mrengo huo utakuwa mwamuzi mkuu kuhusu ikiwa utaibuka mshindi kwenye uchaguzi huo au la.

Kwa sasa, ushauri kwa Bw Musyoka ni kufanya maamuzi ya haraka, ikiwa analenga kujiondoa kwenye baridi la kisiasa tangu mwaka 2013.

[email protected]

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending