Connect with us

General News

Marais wa mataifa ya Afrika Mashariki pia waomboleza Kibaki – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Marais wa mataifa ya Afrika Mashariki pia waomboleza Kibaki – Taifa Leo

Marais wa mataifa ya Afrika Mashariki pia waomboleza Kibaki

NA HILARY KIMUYU

MARAIS na viongozi kutoka mataifa ya Ukanda wa Afrika Mashariki pia wameunga na Wakenya kuomboleza kifo cha rais wa tatu nchini Mwai Kibaki.

Katika risala zake, Rais Yoweri Museveni wa Uganda alimtaja Kibaki kama kiongozi ambaye alionyesha uongozi bora alipokuwa mamlakani.

“Nimepokea habari kuhusu kifo cha Rais Mwai Kibaki kwa huzuni kuu. Kwa niaba yangu na ya watu wa Uganda, natuma risala za pole kwa Rais Uhuru Kenyatta na watu wa Kenya kufuatia kifo cha kiongozi huyo shupavu,” Rais Museveni akasema kupitia mtandao wa Twitter.

Rais Museveni alimiminia sifa Kibaki kwa mchango wake wa kuimarisha uchumi wa Kenya na kupalilia amani Kenya na katika ukanda mzima wa Afrika Mashariki.

Naye Rais Tanzania Samia Suluhu Hassan alimtaja Kibaki kama “kiongozi mahiri na mtumishi bora wa umma”.

“Kwa hivyo, nasikitishwa kabisa na taarifa ya kifo cha Mzee wetu na Rais Mstaafu wa Kenya, Mwai Kibaki,” akaongeza, kwenye taarifa.

Kwa upande wake, Rais Paul Kagame alisema Kibaki atakumbukwa kutoka na rekodi yake nzuri ya kuchochea maendeleo ya kiuchumi ya Kenya na kupalilia utangamano kati ya mataifa ya Afrika Masharika.

“Serikali na wananchi wa taifa la Rwanda wanasimama na Kenya wakati huu wa maomboleza,” akasema, kwenye taarifa.

Ubalozi wa Amerika nchini Kenya pia ulituma risala za rambirambi kwa familia ya Kibaki na taifa la Kenya kwa ujumla.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending