Connect with us

General News

Walimu 22,000 kupata mafunzo ya gredi 6, asema Magoha – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Walimu 22,000 kupata mafunzo ya gredi 6, asema Magoha – Taifa Leo

Walimu 22,000 kupata mafunzo ya gredi 6, asema Magoha

NA CECIL ODONGO

WALIMU 22,000 watapokea mafunzo kuwaandaa kuwafundisha wanafunzi katika sekondari ya chini ambayo itaanza Januari 2023. Mafunzo hayo yatakuwa yakilenga walimu 60,000 kufikia Januari mwaka ujao kutoka shule za umma na za kibinafsi.

Kwa mujibu Waziri wa Elimu Profesa Magoha, mtaala huo utaendelea kutekelezwa huku wanafunzi waliouanzisha wakitarajiwa kujiunga na Gredi ya Sita shule zikifunguliwa kesho Jumatatu.

“Kuna zaidi ya wanafunzi milioni tisa ambao sasa wanapokea mafunzo ya CBC. Serikali inaendelea kujizatiti kuhakikisha kuwa kuna miundomsingi hasa madarasa ambayo yanakidhi idadi kubwa ya wanafunzi,” akasema Profesa Magoha.

Tayari serikali inatarajia kukamilisha ujenzi wa madarasa 6,470 kufikia mwisho wa mwezi huu wa Aprili.

Madarasa hayo yatatumiwa na wanafunzi wa shule ya upili ya kiwango cha kwanza chini ya CBC.

Kwa kuwa serikali ilikuwa ikilenga madarasa 10,000, ujenzi wa mengine 3,530 yaliyosalia utamalizika kati ya Mei na Agosti 2022.

Serikali ilianza kutekeleza mtaala huo mnamo 2016 lakini imekosolewa na baadhi ya wanasiasa na wazazi, wakisema kuwa gharama ya utekelezaji wake ni kubwa hasa kwa wazazi nyakati hizi ngumu za kiuchumi.