Connect with us

General News

DCI wachunguza kifo cha mwanawe mbunge maalum – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

DCI wachunguza kifo cha mwanawe mbunge maalum – Taifa Leo

DCI wachunguza kifo cha mwanawe mbunge maalum

ROBERT KIPLANGAT NA KNA

MAAFISA wa Idara ya Kupeleleza Uhalifu (DCI) Jumanne walifika nyumbani kwa mbunge wa kuteuliwa, David Ole Sankok, eneo la Ewuaso Ngíro, Kaunti ya Narok kurekodi taarifa kuhusiana na kifo cha mwanawe.

Inadaiwa kuwa mwanawe wa miaka 15 alijiua kwa kujipiga risasi mnamo Jumatatu alasiri akitumia bunduki ya babake.

“Risasi ilipitia kidevuni na kutokea kwenye sehemu ya juu ya kichwa,” alisema Kamanda wa Polisi katika Kaunti ya Narok, Kizito Mutoro.

Maafisa wa DCI walikusanya taarifa kutoka kwa wafanyakazi wa hoteli ya Bw Sankok ya Osim County Lodge, ambayo ipo mita mia moja kutoka kwa eneo la tukio.

Habari zilisema Bw Sankok alikuwa katika hoteli ya Osim akihudhuria mkutano wa kisiasa kisa hicho kilipotokea.

Inasemekana kuwa kijana huyo na babake walikuwa na ugomvi mkali baada yake kukataa kurejea shuleni.

Rafiki wa karibu kwa familia hiyo, Bw George Kariuki, alieleza kuwa marehemu alikuwa kijana mpole na mwenye maono pevu.

“Nilikuwa naye juzi na hakuonyesha dalili za kusongwa na mawazo. Nimehuzunishwa na kifo chake,” alieleza Bw Kariuki.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending