[ad_1]
Abraham na Smalling waongoza AS Roma kukomoa Atalanta katika Serie A
Na MASHIRIKA
TAMMY Abraham alifunga mabao mawili naye Mwingereza mwenzake Chris Smalling akapachika wavuni goli jingine katika ushindi wa 4-1 uliosajiliwa na AS Roma dhidi ya Atalanta katika Ligi Kuu ya Italia (Serie A) mnamo Jumamosi.
Abraham ambaye ni fowadi wa zamani wa Chelsea, alifungulia Roma ukurasa wa mabao baada ya sekunde 57 kabla ya kufunga bao la nne la Roma. Ufanisi huo ulifikisha idadi ya mabao yake hadi 12 kufikia sasa msimu huu.
Smalling alifunga bao lake katika dakika ya 72 baada ya Nicolo Zaniolo kufanya mambo kuwa 2-0 na kabla ya Abraham kuzamisha kabisa chombo cha wenyeji wao mwishoni mwa kipindi cha pili.
Bryan Cristante wa Roma alijifunga kabla ya kipenga cha kuashiria mwisho wa kipindi cha kwanza kupulizwa. Jose Luis Palomino alidhani alikuwa amesawazishia Atalanta kwa kufanya mambo kuwa 2-2 katika dakika ya 56 ila ikabainika kwamba alicheka na nyavu za Roma akiwa ameotea.
Chini ya kocha Jose Mourinho, Roma kwa sasa wanakamata nafasi ya tano jedwalini kwa alama 31 sawa na Juventus waliotandika Bologna 2-0 kupitia mabao ya Alvaro Morata na Juan Cuadrado.
MATOKEO YA SERIE A (Jumamosi):
Atalanta 1-4 AS Roma
Bologna 0-2 Juventus
Cagliari 0-4 Udinese
TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO
[ad_2]
Source link