Connect with us

General News

Achani akanusha kuwatenga wanawake wanaosaka nyadhifa za kisiasa – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Achani akanusha kuwatenga wanawake wanaosaka nyadhifa za kisiasa – Taifa Leo

Achani akanusha kuwatenga wanawake wanaosaka nyadhifa za kisiasa

NA SIAGO CECE

NAIBU Gavana wa Kwale, Bi Fatuma Achani, amekanusha madai ya wapinzani wake kwamba hajajitolea kusaidia wanawake wanaotaka kuwania viti vya kisiasa.

Akizungumza katika warsha ya kuhamasisha wanawake kujitokeza kwa wingi kuwania viti katika uchaguzi ujao, Bi Achani alisisitiza kuwa hajawahi kumwekea mwanamke yeyote vikwazo kisiasa.

Bi Achani amelenga kuwania ugavana katika kaunti hiyo, ambapo Gavana Salim Mvurya anaelekea kukamilisha kipindi chake cha pili uongozini.

“Mimi naunga kila mwanamke ambaye anataka kiti chochote na ndiyo maana hutawahi kunisikia nimesimama nakibishana na mwanamke mwenzangu,” Bi Achani alisema.

Wakati huo huo, alihimiza wanawake wasisuburi hadi dakika ya mwisho ili kuwania viti.

Aliwataka wanawake walio na maazimio ya kujitosa katika siasa, wawe wakishiriki katika masuala ya kijamii ili kutangamana kwa karibu na wananchi hata kabla ya kuingilia siasa.

“Kina mama wenzangu ambao wanataka hivi viti, usingoje dakika ya mwisho ndipo ujitolee kuwa unataka hivi viti. Kuwa na wananchi kwa karibu na ukiishi na wananachi kama vile walivyo, hautakuja kulaumu mwenzako ukisema mbona mimi sipewi,” Bi Achani alisema.

Katika warsha hiyo, wanawake katika Kaunti ya Kwale, walihimizwa kujitokeza kwa wingi ili kuwania nafasi zaidi za uongozi katika uchaguzi ujao.

Kulingana na shirika la kutetea haki za kibinadamu la Human Rights

Agenda (HURIA), idadi ya wanawake katika kaunti hiyo ambao wanawania nyadhifa mbalimbali za kisiasa, bado iko chini.

Afisa wa mipango katika shirika hilo, Bi Mwinyihaji Chamosi, alisema kuwa tayari wameanzisha mpango wa kuwahamasisha wanawake kuhusu umuhimu wa kuwania nyadhifa hizo.

“Tunataka kuhakikisha kuwa kina mama wanahusika katika mambo ya uchaguzi, na pia wanachukua vyeo ili waweze kuongoza,” Bw Chamosi alisema.