Connect with us

General News

Afisa bandia wa polisi asukumwa jela miezi sita – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Afisa bandia wa polisi asukumwa jela miezi sita – Taifa Leo

Afisa bandia wa polisi asukumwa jela miezi sita

NA RICHARD MUNGUTI

AFISA bandia wa polisi aliyewateka nyara wanahabari wawili akiwamo mwanamke katika Mahakama Kuu ya Milimani amefungwa jela miezi sita bila faini.

Akimfunga Alex Oyula Baraza, hakimu mwandamizi Bernard Ochoi alisema “mshtakiwa alikuwa na nia mbaya alipodanganya walinzi katika jengo la mahakama kwamba yeye ni afisa wa polisi kutoka kitengo cha uchunguzi wa jinai (DCI).”

“Ijapokuwa mahakama imeelezwa mshtakiwa ni mkosaji wa mara ya kwanza, anastahili adhabu kali kwa vile alihatarisha maisha ya mabawabu katika jengo la mahakama na watu wengine wanaofika kortini kwa ajili ya shughuli mbalimbali,” alisema Bw Ochoi.

Mfungwa huyo aliwadanganya mabawabu katika lango nambari 4 kwamba ni afisa kutoka DCI na alikuwa amefika mahakamani kuwachukua mahabusu.

Punde si punde alionekana akiandamana na wanahabari wawili aliowadanganya alitaka waandamane naye wakapige picha akimtia nguvuni mshukiwa katika jengo la Afya Centre.

Baraza alikiri mbele ya Bw Ochoi aliwahadaa wanahabari wawili Gladys Nzisa Musyoka (wa Mbaitu FM) na Cyrus Sila Kimanga (Uzalendo Media) kwamba angelitaka waandamane naye wakapige picha akimtia nguvuni mshukiwa katika jengo la Afya Centre barabara ya Tom Mboya, Nairobi.

Baraza alikiri alitekeleza uhalifu huo katika Mahakama Kuu Milimani Nairobi mnamo Machi 1, 2022.

Kiongozi wa mashtaka James Gachoka alieleza mahakama Baraza alikuwa na nia fiche alipotoa habari za uwongo kwa walinzi na polisi kortini.

Baraza alikamatwa na walinzi wa kampuni ya Gyto Security Ltd wakiondoka na wanahabari hao.

Mshtakiwa alikuwa amewaingiza ndani ya gari lakini akazuiliwa katika lango na bawabu na kuulizwa “ikiwa mahabusu ni wanahabari hao.”

Polisi huyo bandia alipewa siku 14 kukata rufaa.