Connect with us

General News

Afisi aliyofungua Ruto yakosa polisi – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Afisi aliyofungua Ruto yakosa polisi – Taifa Leo

Afisi aliyofungua Ruto yakosa polisi

NA RUTH MBULA

AFISI moja ya polisi iliyofunguliwa na Naibu Rais William Ruto kwenye ziara ya mwisho aliyofanya katika Kaunti ya Nyamira, bado haijapokea polisi yeyote hadi sasa.

Afisi ya Bomwagamo, iliyojeng – wa kupitia Hazina ya Ustawishaji wa Maeneobunge (NG-CDF) ya eneo la Mugirango Kaskazini imebaki hivyo tu, bila kuendesha shughuli zozote.

Afisi hiyo ambayo iko karibu na afisi ya chifu ya Itibo, ilifunguliwa rasmi Novemba mwaka uliopita na Dkt Ruto. Maafisa wa ngazi za juu wa polisi hawakuhudhuria hafla hiyo.

Kamishna wa Kaunti ya Nyamira, Bw Michael Lesimam, aliiambia Taifa Leo kwamba serikali haiwezi kuwatuma polisi katika afisi hiyo kwani Kamati ya Kaunti kuhusu Usalama haikushauriwa kuhusu mradi huo.

“Hakuna vyoo hapo. Ni vipi polisi watafanya kazi katika eneo kama hilo?” akaeleza Bw Lesimam.

Alisema kuna masuala kadhaa ambayo lazima yazingatiwe kabla ya taasisi za kiusalama kujengwa.

Alieleza kuwa kuna haja ya

wataalamu kujumuishwa, kwani majengo kama maeneo ya kuwekea silaha lazima yajengwe kwa muundo maalum.

Alisema kuna uhaba mkubwa wa maafisa wa usalama, hivyo seri – kali inayapa kipao mbele maeneo yanayokumbwa na tishio za kiusalama.

Hata hivyo, mbunge wa eneo hilo, Joash Nyamoko alipuuzilia mbali hatua ya serikali akisema “afisi hi – yo ilijengwa ili kurahisisha taratibu za kiusimamizi.” Majibizano hayo yanajiri huku Dkt Ruto akitarajiwa kuzuru katika eneo hilo leo.

Dkt Ruto anatarajiwa kumtangaza mbunge wa Nyaribari Masaba, Ezekiel Machogu, kama mwakilishi wake wa kisiasa katika eneo hilo.

Bw Machogu analenga kuwania ugavana katika Kaunti ya Kisii. Mbunge huyo amekuwa akitaja ukosefu wa uungwaji mkono wa serikali kwenye miradi kama sababu iliyomfanya kuhamia katika kambi ya Dkt Ruto.

“Hakuna shughuli zozote zinazoendelea katika Kituo cha Polisi cha Ichuni ambacho nilijenga kwa kutumia fedha za CDF kwani serikali bado haijawatuma polisi,” akasema.

Afisi hizo mbili ni sehemu ya mi – radi mingi iliyozinduliwa na Dkt Ruto nchini lakini imekosa kutumika kutokana na mivutano ya kisiasa ambayo imekuwepo katika utawala wa Jubilee.

Maafisa wakuu wa serikali wamekuwa wakisema Dkt Ruto huwa hashauriani na wizara husika kabla ya kuzindua miradi hiyo.

Akihutubu Jumatatu wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Afya Bora kwa Wote jijini Mombasa, Rais Uhuru Kenyatta alimkosoa vikali Dkt Ruto kwa kuendeleza kampeni za mapema.

Rais alimlaumu Dkt Ruto kwa kuendeleza kampeni akiwa juu ya magari badala ya kufanya kazi.

Lakini akihutubu kwenye mikutano kadhaa Jumanne katika Kaunti ya Kakamega, Dkt Ruto alipuuzilia mbali kauli ya Rais Kenyatta akisema hakuna kosa lolote kwake kusimama juu ya magari.

Desemba mwaka uliopita, Dkt Ruto alizindua Kituo cha Polisi katika Kaunti ya Nakuru, hali iliyokosolewa na aliyekuwa Mshirikishi Mkuu wa Bonde la Ufa, George Natembeya.