Connect with us

General News

Afisi mpya ya chifu wa Thika kuanza kutumika – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Afisi mpya ya chifu wa Thika kuanza kutumika – Taifa Leo

Afisi mpya ya chifu wa Thika kuanza kutumika

NA LAWRENCE ONGARO

MJI wa Thika umepata afisi mpya ya chifu ikiwa hatua nojawapo ya kuleta huduma karibu na wakazi.

Hapo awali wakazi wa Thika walilazimika kutembea kilomita tano hivi kwenda kwa chifu ili kutatua shida zao.

Mbunge wa Thika Bw Patrick ‘Jungle’ Wainaina alieleza kuwa sehemu ambayo afisi hiyo imejengwa ilikuwa imenyakuliwa lakini serikali ilirejesha kipande hicho cha ardhi kwa umma ili afisi ya chifu ijengwe hapo.

“Eneo hilo lilikuwa limenyakuliwa na lakini serikali ifanya juhudi kuregesha ardhi hiyo kwa wananchi,” alifafanua mbunge huyo.

Alieleza kuwa afisi mpya iliyojengwa itakuwa na umuhimu wake kwani imejengwa katikati mwa mji wa Thika.

Afisi mpya ya chifu ni ya kisiasa ambayo imegharimu takribani Sh3 milioni kukamilika.

Mbunge wa Thika alipongeza juhudi hizo za kujengwa kwa afisi hiyo ambayo ilifadhiliwa na pesa za maendeleo za NG-CDF.

“Afisi yenyewe ni ya kisasa ambapo imewekwa vifaa vya teknolojia ya sasa kama vipatakilishi ambapo mambo yote yataendeshwa kidijitali. Hata wananchi wamepongeza hatua hiyo,” alisema mbunge huyo.

Alieleza kuwa pia kuna chumba cha wageni ambacho kina viti vya kisasa vya kukalia.

Alitoa wito kwa wananchi watakaohudumiwa wawe na ushirikiano mzuri na chifu wa Thika Bw Simon Kamau.

Bw Kamau alisema afisi mpya itawapa wananchi nafasi nzuri ya kufika hapo haraka.

“Ninatoa wito kwa wananchi wafike afisini wakati wowote wanapopata shida ili iweze kutatuliwa mara moja,” alifafanua chifu huyo.

Alisema yeye kama mtumishi wa umma atajitahidi kuona ya kwamba kila mmoja anapata huduma wakati wowote bila kubaguliwa.

Bw John Kimani mkazi wa mji wa Thika, alipongeza hatua hiyo ya kufungua afisi mpya akisema anaamini itarahisisha kazi ya kila mmoja.

“Hapo awali tulilazimika kutembea mwendo mrefu kutafuta usaidizi wa chifu, lakini sasa mambo yatakuwa rahisi,” alisema Bw Kimani ambaye ni mfanyakazi katika mji wa Thika.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending