Connect with us

General News

Ahadi hewa ya Raila kuwapa makao waathiriwa wa ghasia za 2007 – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Ahadi hewa ya Raila kuwapa makao waathiriwa wa ghasia za 2007 – Taifa Leo

TUSIJE TUKASAHAU: Ahadi hewa ya Raila kuwapa makao waathiriwa wa ghasia za 2007

NA CHARLES WASONGA

KIONGOZI wa ODM Raila Odinga ameahidi kuwapa makao waathiriwa wa ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa 2007, endapo atachaguliwa kuwa rais mwaka huu.

Lakini asije akasahau mnamo 2009 serikali ya muungano, almaarufu nusu-mkate, ambayo yeye na Rais mstaafu Mwai Kibaki waliongoza, ilitoa ahadi sawa na hiyo aliyotoa mjini Nakuru Jumatano wiki hii. Lakini haikutimiza.

Serikali hiyo, ambayo Bw Odinga aliihudumia kama Waziri Mkuu, pia iliahidi kuwapa wakimbizi wa ndani kwa ndani (IDPs) 300,000 fidia ya Sh50,000 kila mmoja. Lakini shughuli ya utoaji fidia hiyo ilizongwa na ufisadi.

Serikali ya Jubilee ilirithi shida hiyo ilipoingia mamlakani 2013 na ikaweza kuwapa baadhi ya IDPs 200,000 makao mbadala.

Hata hivyo, Novemba mwaka jana, mshirikishi wa muungano wa wakimbizi hao kaunti ya Nakuru Lucy Njeri alidai wengi wa wanachama wake hawakupokea ardhi mbadala wala fidia ya Sh5,000.