Connect with us

General News

Al-Shabaab saba kushambulia Kenya – ripoti mahakamani – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Al-Shabaab saba kushambulia Kenya – ripoti mahakamani – Taifa Leo

Al-Shabaab saba kushambulia Kenya – ripoti mahakamani

NA BRIAN OCHARO

RIPOTI ya kijasusi iliyowasilishwa katika mahakama ya Mombasa inaonyesha wanamgambo wa Al-Shabaab wamewatuma wapiganaji saba kutekeleza shambulio la kigaidi nchini.

Mahakama ilielezwa Jumatano kuwa, shambulio hilo, linapangwa na wanamgambo hao, ambao tayari wameingia nchini kisiri.

“Ripoti za kijasusi zinaonyesha wanamgambo saba walitumwa kutoka Somalia baada ya likizo ya Pasaka,” akasema Kiongozi wa Mashtaka Hillary Isiaho.

Ufichuzi ulitokea baada ya kukamatwa kwa watu watatu na maafisa wa Kitengo cha Polisi cha Kupambana na Ugaidi (ATPU), ambao walisema wamekuwa katika mawasiliano ya mara kwa mara na wanamgambo hao ambao tayari wameingia Kenya kutekeleza shambulio hilo.

Huku akitegemea hati iliyotayarishwa na ATPU, Bw Isiaho alimwelezea Hakimu Mkazi Mkuu wa Mombasa Vincent Adet kwamba watatu hao wanachunguzwa kwa kuwa katika mawasiliano na wanamgambo hao.

Watatu hao ni Osman Mohamed Hassan, Mohamed Ibrahim Hassan na Hussein Ibrahim Hassan.

“Watuhumiwa walikuwa wakiwasiliana mara kwa mara na magaidi hao (saba),” alisema Bw Isiaho.

Watatu hao walikamatwa Aprili 13, katika duka la Muzamil eneo la Kisauni na kuwekwa rumande katika vituo vitatu tofauti vya polisi vya Makupa, Central na Port.

Washukiwa hao walipatikana na simu nne za mkononi.

Polisi wanasema uchunguzi wa awali umebaini kuwa watatu hao wana uhusiano wa kifamilia na magaidi nchini Somalia.

Bw Mohamed Ibrahim Hassan anaaminika kuwa Raia wa Somalia, ambaye aliingia nchini kwa misheni isiyojulikana.

“Wakati wa kukamatwa kwake, mshtukiwa alikuwa katika harakati za kupata usajili wa Wakenya,” alisema Isaiho.

Huku akiomba ruhusa ya kuwazuilia watatu hao kwa siku 14, Bw Isiaho alisema wapelelezi wanahitaji muda zaidi kufahamu asili na nia zao kupitia kwa mahojiano.

Alisema uchunguzi huo utahusisha kutembelea kambi za wakimbizi za Dadaab na IFO katika kaunti ya Garissa, ambapo Mohamed Ibrahim Hassan anaaminika kukutana na magaidi hao.

“Pia, ninafuata ripoti za kijasusi ili kukamata washukiwa wengine zaidi, ambao wako ndani na nje ya kaunti ya Mombasa,” afisa mpelelezi Jackson Katana alisema.

Mahakama iliambiwa kuwa watatu hao wanachunguzwa kwa kuwa wanachama wa kundi la kigaidi na kuwa na vipengee vinavyohusiana na vitendo vya kigaidi.

Watatu hao hawakupinga ombi la kuwazuilia lakini waliiomba mahakama ipunguze hadi siku saba.

“Polisi wamekuwa na wiki nzima ya kufanya uchunguzi tangu tulipokamatwa Aprili 13. Waruhusiwe kutuzuilia kwa wiki moja pekee,” alisema Bw Osman.

Aidha alilalamika kuwa alifunga biashara yake kwa muda wote tangu kukamatwa hivyo amekuwa akipata hasara.

Kesi hiyo itatajwa tena Mei 5.