Connect with us

General News

Aliyejaribu kumuua Kosewe asema alikuwa akijikinga – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Na RICHARD MUNGUTI

MFANYABIASHARA anayekabiliwa na shtaka la kujaribu kumuua mmiliki wa hoteli ya Ronalo Foods almaarufu Kosewe wakizozania mwanamke Jumatatu aliomba aachiliwe huru akidai alimjeruhi akijitetea.

Kupitia kwa wakili Prof Tom Ojienda , Tom Mboya alimsihi hakimu mkuu Martha Mutuku amwachilie huru ama amuonye asirudi kutumia vibaya silaha.“Mboya alimfyatulia risasi William Osewe akijikinga. Alimchapa risasi ya mkono kusudi aangushe bastola aliyokuwa ameshika mkononi akimwelekezea,” alisema Prof Ojienda alisema.

Wakili huyo mwenye tajriba ya juu alieleza mahakama kuwa kiini cha mzozo kati ya wawili hao ni mwanamke tu.“Osewe yuko na uhasama mkali na mshtakiwa. Anadai kuwa Mboya yuko na uhusiano wa kimapenzi na mkewe. Jambo hili limesheheni kwa muda mrefu,” alisema Prof Ojienda.

Wakili huyo alimweleza hakimu kiini cha uhasama huo ni madai hayo ya uhusiano wa kimapenzi kati ya Mboya na mkewe Osewe.“Hata mlalamishi (osewe) aliwahi mshtaki Mboya kortini kuhusu suala hili,” Prof Ojienda.

Mahakama ilielezwa mnamo Desemba 16 2016 katika hoteli ya Argon mshtakiwa aliandamwa na Osewe.“Mshtakiwa alipomwona Osewe alijua ameisha.Alijua atauawa kwa vile amekuwa akimwinda,” Prof Ojienda.

Mahakama ilielezwa mshtakiwa hakuwa na budi ila kujikinga.Mahakama iliombwa imwachilie kwa vile hakuwa na nia ya kuua mlalamishi.Prof Ojienda alieleza mahakama mshtakiwa alikuwa rafikiye Osewe.Lakini Osewe aliyekuwa ameketi kortini kufuata kesi hiyo alimkatiza Prof Ojienda na kusema “Mboya sio rafiki yangu.

Sikuwa na bastola siku ile aliponishambulia.Alitaka kuniangamiza.” Lakini kiongozi wa mashtaka Bw Anderson Gikunda aliomba mahakama imwadhibu vikali Mboya kwa vile alikuwa na nia ya kuwaua Osewe na mlinzi katika hoteli hiyo aliyechapwa risasi ya mguu.Osewe alijeruhiwa na anatembea akitumia mkogojo.Mboya atahukumiwa Agosti 7, 2021.

Aliyejaribu kumuua Kosewe asema alikuwa akijikinga – Taifa Leo
William Osewe (mwenye mikogojo)

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Trending