–Zacharia Kimani Mwaura alidai kuwa maafisa sita wa polisi ambao walimkamata walimpora simu mbili na KSh72,000
– Mwaura anakabiliwa na shtaka la kujitambulisha kwa inspekta wa Kituo cha Polisi cha Thika kama Ndolo na kumuagiza amkamate mfanyabishara mmoja
– Mwaura aliachiliwa huru kwa dhamana ya KSh100,000 na Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Makadara
Jamaa mmoja ambaye anatuhumiwa kwa kujifanya kamanda wa polisi eneo la Nairobi, Philip Ndolo na kuamuru kukamatwa kwa mfanyabiashara mmoja sasa anawakashifu polisi kwa kuiba KSh72,000 na simu ya kudurusu nyumbani kwake.
Zacharia Kimani Mwaura alidai kuwa maafisa sita wa polisi ambao walimkamata, walifanya msako nyumbani kwake na kuondoka na pesa hizo na simu.
Koplo Esha Buya kutoka Idara ya Upelelezi afisi za Kasarani, alisema hakufahamu kisa hicho na pia hakuwa miongoni mwa maafisa ambao waliendesha msako huo.
Mwaura anakabiliwa na shtaka la kujipendekeza kwa inspekta Samuel Kyulu wa Kituo cha Polisi cha Thika kama Ndolo.
Mwauru anakabiliwa na shtaka la kujifanya kamanda wa polisi eneo la Nairobi, Philip Ndolo. Picha: UGC. Source: UGC
Mshukiwa huyo anadaiwa kumpigia Kyulu simu mnamo Februari, 20, 2020 na kumuagiza awakamate washukiwa fulani kuhusiana na kesi nambari OB57/20/2/2020 iliyowasilishwa stesheni humo.
Hata hivyo, alikanusha madai hayo mbele ya Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Makadara Heston Nyaga.
Mwaura alifikishwa mbele ya Mahakama ya Makadara kujibu mashtaka. Picha: Daily Nation. Source: UGC
Kisa hiki kilitokea wakati Ndolo alikuwa nje ya nchi kwa shughuli rasmi kama ilivyoripoti Nairobi News.
Katika hati ya kiapo iliyowasilishwa mahakamani Februari 24,2020, Buya alieleza kuwa polisi walipata simu mbili nyumbani kwa Mwaura, ambazo wanashuku zilitumika katika uhalifu huo.
Hakimu Nyaga aliwataka Stanley Gitonga na Daniel Nyamuhanga, ambao ndio walimkamata mshukiwa wafike mbele yake mnamo Jumatano, Julai 27, wakati kesi hiy itatajwa.
Nyaga pia alimuachilia Mwaura huru kwa dhamana ya KSh100,000.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.