Connect with us

General News

Aliyetajwa wa pili bora kwa walemavu abainika si mlemavu – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Aliyetajwa wa pili bora kwa walemavu abainika si mlemavu – Taifa Leo

#KCPE2021: Aliyetajwa wa pili bora kwa walemavu abainika si mlemavu

BRIAN OCHARO NA FARHIYA HUSSEIN

FAMILIA ya mwanafunzi aliyetajwa wa pili bora kitaifa kati ya watahiniwa wenye mahitaji maalumu, amebainika kuwa si mlemavu.

Waziri wa Elimu, Prof George Magoha, alikuwa amemtangaza Grace Neema Katana kutoka Shule ya Msingi ya Havilah iliyo Mtwapa, Kaunti ya Kilifi, wa pili kwenye orodha hiyo kwa kupata alama 407.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Bw Erick Kai, na mamake mwanafunzi huyo, Bi Joyce Furaha, walithibitisha kwamba yeye si mlemavu wakishangaa alivyoingizwa kwa orodha hiyo.

‘Mtoto wangu si mlemavu. Amesomea katika shule hii tangu darasa la nne na hana tatizo lolote,’ akasema Bi Furaha.

Bw Kai alisema shule hiyo ni ya kibinafsi na hukubalia watoto wenye ulemavu ambao huwa hawatengwi na wengine, lakini akasisitiza Grace si mlemavu.

Alisema kuna uwezekano maelezo kumhusu yalisajiliwa na makosa.

Philip Karani kutoka Likoni School for the Blind, aliibuka nafasi ya nane kwa alama 397 katika orodha ya wanafunzi walemavu kitaifa.

Nafasi ya kwanza ilimwendea Bethany Tahillah Migosi wa shule ya Thorn Grove Academy ambaye alipata alama 417.

Kwenye mahojiano na Taifa Leo, Karani alisema matokeo hayo yamemtia moyo kutia bidii zaidi maishani.

Mvulana huyo mwenye umri wa miaka 16 alisema angelipenda kwenda Shule ya Upili ya Thika kisha baadaye asomee uhasibu.

Mamake, Bi Phedes Njoki, na mwalimu mkuu wa shule alikosomea, Bi Elizabeth Ngare, walitaja matokeo yake kama muujiza.