Connect with us

General News

Amri wakazi wa ‘Bangladesh’ wahame kupisha stima – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Amri wakazi wa ‘Bangladesh’ wahame kupisha stima – Taifa Leo

Amri wakazi wa ‘Bangladesh’ wahame kupisha stima

NA WACHIRA MWANGI

MAELFU ya wakazi wa eneo lisilo rasmi la Bangladesh, Mombasa wameamrishwa wahame kwenye barabara kuu ambapo kuna nguzo za umeme ili kuwalinda dhidi ya hatari.

Mkurugenzi Mkuu wa Kenya Power (KPLC) Kanda ya Pwani, Hicks Waswa, alisema waliojenga kwenye nguzo hizo wako katika hatari kuu.

“Tunaendelea kufanya utafiti ku – husu wezi wa umeme. Eneo la Bangladesh linajulikana sana kutokana na wizi wa umeme. Ni eneo lenye watu wengi sana, wakazi ni maelfu na tayari tumeshawapa notisi ya kuhama,” akasema Bw Waswa.

Kadhalika alisema kuwa wizi wa umeme umekuwa tatizo la kitaifa.

“Hii ndiyo maana mwezi uliopita Waziri wa Usalama, Dkt Fred Matiangi alitoa notisi ya siku 30 kwa watu waliojenga karibu na nguzo hizo wahame kwa kuwa ni hatari kwa maisha yao.” Alisema kutotilia maanani maagizo ya serikali ni jambo ambalo watu wanafaa kuepuka.

“Pindi tu wanapokuwa na habari zaidi, tunakuwa na mazingira bora ya biashara. Kwa sasa tunawashirikisha wakazi wa Changamwe na Bangladesh ili kuhakikisha wote wako salama na tuna usambazaji wa umeme thabiti,” akasema Bw Waswa.

Alibainisha kuwa mkoa huo haujawa na matukio yoyote ya uharibifu wa nyaya za umeme kwa muda wa wiki tatu zilizopita tangu kutekelezwa kwa marufuku ya uuzaji wa vyuma vikuukuu.

“Uharibifu wa nyaya umepungua tangu marufuku ya biashara ya vyuma vikuukuu kutekelezwa. Katika wiki tatu zilizopita, tumeona uthabiti kidogo katika usambazaji wa umeme katika eneo hili,” akasema Bw Waswa.

Hivi karibuni kampuni ya kusambaza umeme nchini (KPLC) ilianza kuweka uzio wa mita kadha ili utumike katika maeneo maalum pekee.

Bw Waswa alibainisha kuwa kampeni ya kukusanya data na taarifa za nambari ya mita na eneo,inaendelea.