[ad_1]
Arteta akiri hajakuwa akimtendea Nketiah haki kwa kumlisha benchi kambini mwa Arsenal
Na MASHIRIKA
MKUFUNZI Mikel Arteta amekiri kuwa “hajakuwa akimtendea haki” fowadi Eddie Nketiah baada ya chipukizi huyo raia wa Uingereza kufunga mabao mawili dhidi ya Chelsea na kusaidia waajiri wake kusajili ushindi wa 4-2 mnamo Jumatano usiku ugani Stamford Bridge.
Nketiah, 22, alikuwa akiwajibishwa na Arsenal katika kikosi cha kwanza kwa mara ya pili pekee ligini msimu huu. Kwa kuwa mkataba wake wa sasa na Arsenal unatamatika mwishoni mwa msimu huu, Nketiah amekuwa akilalamikia kutowajibishwa kwake mara kwa mara.
“Nadhani ingekuwa vyema kumchezesha mara kwa mara katika kikosi cha kwanza. Nilimweleza kwamba sijakuwa nikimtendea haki mwishoni mwa mechi dhidi ya Chelsea,” akasema Arteta.
Arsenal wamekuwa katika mazungumzo na Nketiah kuhusu uwezekano wa kurefusha kandarasi yake uwanjani Emirates. Hata hivyo, sogora huyo wa zamani wa Uingereeza U-21 amekuwa akitaka uhakika wa kupangwa mara kwa mara katika kikosi cha kwanza cha Arsenal katika siku za usoni kabla ya kutia saini mkataba mpya.
“Kumekuwa na mazungumzo na ofa ya mkataba mpya. Lakini kubwa zaidi katika maazimio yangu kwa sasa ni kucheza mara kwa mara katika kikosi cha kwanza cha Arsenal. Nakipenda sana kikosi hicho,” akasema Nketiah.
Nketiah amechezeshwa na Arsenal mara saba pekee muhula huu huku gozi dhidi ya Southampton mnamo Aprili 16, 2022 likiwa lake la kwanza ligini msimu huu.
Amekuwa mvamizi chaguo la tatu kambini mwa Arsenal baada ya Alexandre Lacazette na Pierre-Emerick Aubameyang aliyeyoyomea kambini mwa Barcelona mnamo Januari 2022. Kukosekana kwa Lacazette mnamo Jumatano baada ya kuugua Covid-19, kulimpa Nketiah fursa ya kuwa tegemeo la Arsenal katika safu ya mbele.
Mechi dhidi ya Chelsea ilima fursa ya kucheka na nyavu za wapinzani kwa mara ya kwanza tangu afunge bao katika sare ya 1-1 dhidi ya Fulham zaidi ya mwaka mmoja uliopita ligini.
“Ambacho Nketiah amefanya dhidi ya Chelsea ni zao la kile ambacho amekifanya katika kipindi cha miezi 10 iliyopita. Ametudhuhirishia sote kuhusu ukubwa wa uwezo wake uwanjani,” akaongeza Arteta.
TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO
Next article
PSG sasa wanahitaji alama moja kutokana na mechi tano ili…
[ad_2]
Source link