Connect with us

General News

Ashtakiwa kuiba mkokoteni aliodai ulitwaliwa na kanjo – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Ashtakiwa kuiba mkokoteni aliodai ulitwaliwa na kanjo – Taifa Leo

Ashtakiwa kuiba mkokoteni aliodai ulitwaliwa na kanjo

Na RICHARD MUNGUTI

MBURURAJI mkokoteni aliyeomba jirani yake kusafirisha mizigo kisha ukwatwaliwa na askari wa kaunti ya Nairobi ameshtakiwa kwa wizi.

Nelson Omangwa Ondieki aliyeshtakiwa mkokoteni wa Nelson Mutua alieleza hakimu mwandamizi Bi Esther Boke , “sikuiba mkokoteni huo ila ulitwaliwa na askari wa kanjo kisha wakataka niwape hongo ya Sh20,000 ndipo wauachilie.”Ondieki alikabiliwa na shtaka la kuiba mkokoteni huo wa Mutua katika mtaa wa Kangemi Nairobi.

Mkokoteni huo ,mahakama ilielezwa uko na thamani ya Sh7,000.Mshtakiwa alieleza mahakama alikuwa ameomba mkokoteni huo kubeba mizigo katika eneo la Waruku mtaani Kangemi kaunti ya Nairobi. Mshtakiwa alitoweka hadi Novemba 4, 2021 alipoonekana na Mutua.

Mlalamishi (mutua) alimwona mshtakiwa kisha akapiga kamsa na kusaidiwa na wananchi kumtia nguvuni. Mahakamani mshtakiwa alijitetea na kumlilia hakimu amwachilie kwa dhamana. “Askari wa kanjo walinisomba pamoja na mkokoteni na mizigo niliyokuwa nayo.Wamekataa kuuachili huku wakidai hongo ya Sh20,000 ambazo sina hata!,”Ondieki alisimulia kortini.

Mshtakiwa alieleza korti amemweleza mlalamishi kilichojiri lakini “amesisitiza anataka mkokoteni wake.” Hakimu alimwachilia kwa dhamana ya Sh200,000 na mdhamini mmoja wa kiasi sawa na hicho ama alipe dhamana ya pesa tasilimu Sh7,500 ndipo aachiliwe.

Kesi hiyo itatajwa Novemba 22,2021.

 

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending