[ad_1]
Asike imani tele Tusker itaibwaga Homeboyz
Na CECIL ODONGO
NAHODHA wa Tusker Eugene Asike ameeleza imani yake kuwa timu hiyo itatamatisha rekodi ya kutoshindwa ya Kakamega Homeboyz msimu huu katika mechi ya Ligi Kuu ugani Bukhungu leo.
Mechi hiyo itaanza saa tisa mchana na itakuwa ya mwisho ligini kabla ya timu hizo kuungana na nyingine kwenye mapumziko wakati wa Krismasi. Ligi itarejelewa Disemba 29/30 lakini itaenda mapumzikoni tena kabla ya kurejea wikendi ya kwanza ya Januari 2022.
Dhidi ya Homeboyz, Asike anaamini kuwa wataipiga Homeboyz kwa kuwa maandalizi yao yamekuwa mazuri na pia wanalenga kupata matokeo mazuri ili kufikia timu zilizoko juu yao katika msimamo mwa jedwali la ligi.“Itakuwa mechi ngumu ikizingatiwa wamekuwa wakisajili matokeo mazuri na pia wapo nyumbani.
Hata hivyo, lazima hata sisi nao tujikakamue kwa sababu tunalenga kufikia timu ambazo ziko juu katika msimamo wa jedwali la ligi,” Asike akaeleza Taifa Leo.Kwa upande wake, mkufunzi wa Kakamega Homeboyz Bernard Mwalala alisema ushindi dhidi ya Gor Mahia wikendi iliyopita ni jambo ambalo washasahau na wanamakinikia kupambana na Tusker.
“Ushindi katika mechi ya leo itashuhudia tukipaa hadi kileleni mwa msimam wa jedwali. Macho yetu na nguvu zetu zote zipo katika kupata ushindi wala hatuna haja na kurejelea ushindi dhidi ya Gor na masuala yaliyozingira mchezo huo,” akasema Mwalala.
Next article
KINYUA BIN KINGORI: Tupokee chanjo kulinda watoto dhidi ya…
[ad_2]
Source link