Connect with us

General News

Asilimia 7 ya viwanda vimefufuka, idadi kubwa yasubiri 2023 – Ripoti – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Asilimia 7 ya viwanda vimefufuka, idadi kubwa yasubiri 2023 – Ripoti – Taifa Leo

Asilimia 7 ya viwanda vimefufuka, idadi kubwa yasubiri 2023 – Ripoti

NA MARY WANGARI

Ni asilimia saba pekee ya biashara nchini ambazo zimeashiria “kufufuka” kwa mazingira yake ya kibiashara kufuatia athari za janga la Covid-19, ripoti mpya imeonyesha.

Idadi kubwa ya biashara katika asilimia 36, zinatumai kupata nafuu na kurejelea hali ya kawaida kuanzia 2023, kulingana na utafiti kuhusu Jukumu Kuu la Fedha (CFO) 4.0 katika Sekta ya Viwanda Kenya, 2021.

Ingawa kuna matumaini makuu kuhusu kuimarika kwa sekta ya viwanda nchini, miongoni mwa wamiliki viwanda mbalimbali vya uundaji na usambazaji bidhaa waliohojiwa katika utafiti huo, ni asilimia moja pekee walioashiria kunawiri kwa biashara zao.

Asilimia 8 ya viwanda havikuonyesha mabadiliko yoyote huku idadi kubwa katika asilimia 50 ikiashiria mazingira mazuri ya kufanya biashara 2021.

Utafiti huo ulifanywa na Shirika la Kimataifa kuhusu Mipangilio ya Raslimali Viwandani, SYSPRO, kwa ushirikiano na Taasisi ya Mahasibu wa Umma Walioidhinishwa Nchini (ICPAK).

Ucheleweshaji katika ununuzi wa raslimali ulitatiza pakubwa shughuli za viwanda nchini kwa asilimia 77 hali iliyoathiri mno sekta ya Vyakula na Vinyaji inayoongoza Kenya, utafiti huo ulisema.

Akizungumza katika uzinduzi wa ripoti hiyo Jumatano, Novemba 24, katika Serena Hotel, Nairobi, Mkuu wa Idara ya Uimarishaji Wateja na Mfumo wa Ikolojia, Bw Doug Hunter, alihimiza wakuu wa viwanda kubuni mikakati itakayoweza kumudu mabadiliko ya siku za usoni.

“Inaashiriwa kuwa Kenya bado ina safari ndefu mbele yake, barabara ambayo ni sharti ipitiwe na viongozi wa siku za usoni wanaosimamia fedha, ambao kwa furaha, tayari wanalenga mikakati bora ya kesho.

“Kwa bahati nzuri idadi kubwa ya biashara hizi zipo katika kiwango cha biashara ndogondogo na kubwakubwa, kumaanisha wadau wa kimataifa wangewezesha kupatikana kwa raslimali katika kipindi cha miezi iliyokuwa migumu zaidi kutokana na janga la Covid-19,” alisema Bw Hunter.

Mkuu wa Idara inayosimamia Utafiti na Maendeleo, ICPAK, Dkt Elizabeth Kalunda, akizungumza katika uzinduzi huo vilevile, alieleza kuwa, japo masuala kadhaa yameathiri kuimarika kwa viwanda nchini, ukosefu wa ufadhili kutoka kwa serikali ulichangia pakubwa.

Ni asilimia 13 pekee ya wamiliki viwanda waliopokea ufadhili kamili kutoka kwa serikali, asilimia 38 nao wakapunguziwa ushuru huku asilimia 51 ya wakikosa kupokea ufadhili.

“Kimataifa, ufadhili huu umechangia mno kuimarisha uwezo wa kampuni kukabiliana na changamoto mpya za Covid-19. Vilevile, misaada hiyo imechangia kuharakisha mageuzi makuu. Kutokana na hilo, Kenya imelazimika kufadhili mageuzi yao kutoka mifukoni mwao, hivyo kusababisha wengi kusitasita kuchukua hatua,” alisema Dkt Kalunda.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending