Rais Uhuru Kenyatta alipokutana na viongozi kutoka Magharibi mwa Kenya. Picha: State House Source: Facebook
Jumatano, Julai moja Atwoli aliungana na magavana kadhaa kutoka eneo hilo na waziri wa Ugatuzi Eugene Wamalwa katika mkutano wa faraghani na Rais Uhuru Kenyatta.
Mkutano huo ulifanyika katika afisi ya Rais ya Harambee House na inaarifiwa ulikuwa wa kupanga maendeleo ya eneo la Magharibi.
Kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi. Mudavadi hakuwa miongoni mwa viongozi kutoka magharibi waliokutana na Rais Uhuru Kenyatta. Picha: ANC Source: UGC
Hata hivyo, kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi na mwenzake wa Ford-Kenya Moses Wetangula hakuwa kwenye mkutano huo.
Kulinga na taarifa iliyotumwa na kitengo cha habari cha rais, viongozi wengine waliohudhuria ni magavana Wycliffe Oparanya (Kakamega), Sospeter Ojaamong wa Busia, Wycliffe Wangamati wa Bungoma, Wilbur Ottichilo wa Vihiga na Patrick Khaemba wa Trans-Nzoia.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.