-Mke huyo alieleza kuwa alimpokea mwanamume huyo kutoka Mombasa kwa mkono mkunjufu akidhania alikuwa mgeni wa mume wake
-Mama huyo wa watoto wanane amekuwa akijistiri kwa nyumba za majirani zaidi ya miaka miwili baada ya wawili hao kuungana pamoja na kumtupa nje pamoja na wanawe
-Wawili hao wanasemekana kuwa wanalala chumba kimoja na kuandamana kama bendera ifuatayao upepo
Mama mmoja mwenye umri wa kati kutoka kijiji cha Sirende, Kaunti ya Trans-Nzoia, analilia haki baada ya mume wake wa zaidi ya miaka 20 kumfurusha nyumbani kwake na kisha kuanza kuishi na mpenzi wake wa kiume.
Millicent Adhiambo, mama ya watoto wanane, alisimulia kuwa kwa zaidi ya miaka miwili amekuwa akilala kwa majirani baada ya mume wake kuanza kuishi na mwanamume huyo kutoka Mombasa.
Adhiambo alidai kuwa mwanamume huyo aliyechukua nafasi yake anatokea Miritini, Mombasa na alimpokea vyema akidhania ni mgeni wa mume wake na kisha baadaye alishirikiana na mume wake kumtupa nje.
“Imekuwa miaka miwili na miezi saba tangu mume wangu anifukuze. Alinitimua na kumleta mwanamume mpenzi wake kutoka Miritini, Mombasa,”
“Wakati mpenzi wake wa kiume aliwasili miaka mitatu iliyopita, nilimpokea vyema nikidhania alikuwa mgeni wa mume wangu.Punde baada ya kuwasili nyumbani kwetu, mume wangu na mpenzi wake walishirikiana kunitupa nje na kubadilisha funguo za nyumba,” Adhiambo aliambia K24.