Connect with us

General News

Balozi wa Kenya nchini Nigeria Dkt Wilfred Machage afariki – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Balozi wa Kenya nchini Nigeria Dkt Wilfred Machage afariki – Taifa Leo

Balozi wa Kenya nchini Nigeria Dkt Wilfred Machage afariki

IAN BRYON na CHARLES WASONGA

BALOZI wa Kenya nchini Nigeria Wilfred Machage amefariki dunia, familia yake imethibitisha Jumamosi, Februari 19, 2022.

Hata hivyo, kakake mwendazake, Sospeter Machage, hakufichua chanzo cha kifo cha Dkt Machage.

Wizara ya Mashauri ya Kigeni nchini pia imethibitisha kifo cha balozi huyo kupitia tovuti yake.

Hata hivyo, ilisema kuwa balozi huyo ambaye zamani alihudumu kama Seneta wa Migori, alikata roho baada ya kula chakula cha mchana jijini Abuja, Nigeria. Hii ni licha ya kwamba alikuwa buheri wa afya.

“Nimejawa na huzuni kubwa kwamba nimempoteza ndugu yangu, rafiki na mshauri mkuu,” Sospeter Machage akasema kwa njia ya simu.

Dkt Machage amefariki akiwa na umri wa miaka 65.

Mwenzake alichaguliwa kwa mara ya kwanza kama mbunge wa iliyokuwa eneobunge la Kuria mnamo 2002. Alihudumu kwa mihula mitatu ambapo alipata fursa ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Waziri Msaidizi katika Afisi ya Makamu Rais.

Mnamo 2013 alichaguliwa kuwa Seneta wa Migori hadi 2017.

Dkt Machage aliteuliwa kuwa balozi wa Kenya nchini Nigeria mnamo Januari 2018.

Baadaye mnamo Julai mwaka huo Dkt Machage alitangaza kuwa amejiondoa katika siasa cha uchaguzi ili aelekeze nguvu na wakati wake katika kuitumikia Kenya kama balozi.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending