[ad_1]
Baraza la Wazee kukagua wagombea viti kabla ya uchaguzi
Na WAWERU WAIRIMU
WAGOMBEAJI wote kutoka jamii ya Wasomali katika Kaunti ya Isiolo watakaguliwa kabla ya kuruhusiwa kugombea viti tofauti vya kisiasa, Baraza la Wazee wa jamii hiyo limesema.
Mwenyekiti wa baraza hilo Shariff Abdullahi alisema kila mgombeaji atakaguliwa na wazee kutoka koo 10 za jamii hiyo ambao watapiga kura ya siri.
Alionya kuwa watakaokaidi mchakato huo hawataungwa mkono na jamii hiyo uchaguzini.Mchakato huo ambao ni sehemu ya demokrasia ya maelewano, unaendeshwa na wazee 30 kila ukoo ukiwakilishwa na wajumbe watatu.
“Yeyote anayetaka kuongoza jamii anafaa kuelewa kuwa kura ya siri ndiyo itatumiwa kuteua wagombeaji wote wakiwemo wanaotaka kuwa manaibu wa magavana,” alisema Bw Abdullahi mnamo Jumamosi wakati wa kuwachagua wagombeaji wa kuwakilisha jamii katika wadi za Burat na Bulapesa.
Bw Mohammed Barre Ahmed na Ismail Jama Sufi watagombea viti vya MCA katika wadi za Burat na Bulapesa.
Next article
TAHARIRI: Viongozi wa kidini watumie fursa hii kuhubiri…
[ad_2]
Source link