Connect with us

General News

Benki Kuu yapanga kupunguza ada za kutuma pesa – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Benki Kuu yapanga kupunguza ada za kutuma pesa – Taifa Leo

Benki Kuu yapanga kupunguza ada za kutuma pesa

NA BRIAN AMBANI

WANANCHI watapata afueni kutokana na hatua ya Benki Kuu ya Kenya (CBK) kupendekeza kupunguza ada za kutuma na kupokea fedha kupitia mtandao mpya wa kidijitali na simu za mkononi.

Nazo kampuni za mawasiliano na benki zinazoendesha huduma hizo zitapata pigo kwani hatua hiyo itazipunguzia mapato.

CBK inasema mfumo wake wa kidijitali kwa jina, “Central Bank Digital Currency (CBDC)” utakuwa ukilenga kupunguza gharama ya huduma za kifedha kupitia

mtandao huo.

“Ikiwa CBK haitatoza ada zozote kwa huduma za CBDC, itaimarisha shughuli za kutuma na kupokea viwango

vidogo vya pesa kwa gharama ya chini kuliko hali ilivyo sasa,” CBK ikasema katika taarifa kuhusu mpango wake wa huduma za fedha kidijitali. Benki hiyo ilisema japo matumizi ya huduma za kupokea na kutuma pesa kwa njia ya simu zimekolea nchini, kuna watu ambao hawatumii huduma hizo kutokana na ada za juu zinazotozwa.

“Mapendekezo yametolewa kwamba kuanzishwa kwa mtandao wa CBDC kutawezesha watu wengi kufikia huduma za kufanya malipo kidijitali. Kwa hivyo, ipo haja ya kupunguza gharama ya huduma hiyo,” CBK ikasema.