Connect with us

General News

Biashara ya vyuma yanoga licha ya marufuku – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Biashara ya vyuma yanoga licha ya marufuku – Taifa Leo

Biashara ya vyuma yanoga licha ya marufuku

GEORGE ODIWUOR NA STANLEY NGOTHO

LICHA ya Rais Uhuru Kenyatta kupiga marufuku uuzaji wa vyuma vikuukuu, biashara hiyo ingali inaendelea kaunti ya Homa Bay.

Hata hivyo, serikali imewaonya vikali watu wanaoendeleza biashara hiyo katika eneo hilo huku uharibifu wa muundomsingi muhimu wa umma ukiendelea.

Rais Kenyatta aliagiza biashara hiyo kusimamishwa lakini wahalifu bado wanavunja miundomsingi kupata vyuma.

Katika Kaunti ya Homa Bay, kuna genge linaloendelea kuharibu mali ya umma na kuuza vyuma kwa wafanyabiashara wanaovinunua na kuviuza.

Wezi hao wanaosemekana kuhudumu kaunti za Kisii, Homa Bay na Kisumu, wanalenga vyuma vinavyotumiwa kujenga barabara.

Pia, wanaharibu transfoma zinazotumiwa na kampuni ya Kenya Power na taa za sola zilizowekwa na serikali ya Kaunti ya Homa Bay.

Kamishna wa Kaunti ya Homa Bay, Bw Moses Lilan alisema kwamba genge hilo limeharibu vyuma vya usalama barabarani katika miji mikubwa katika ukanda wa ziwa.

Vitendo vyao vimeweka hatarini maisha ya madereva na watu wanaotembea kwa miguu.

Vyuma vya usalama katika barabara ya Ahero-Isebania vimeibwa sawa na vilivyoko kwenye daraja la Mbita lililogharimu Sh1.5 bilioni kujenga.