[ad_1]
Binamu ya Uhuru amkosoa kuhusu kuidhinisha Raila
NA MWANGI MUIRURI
BINAMUYE Rais Uhuru Kenyatta amemkosoa kiongozi wa taifa akisema hatua yake ya kumuunga mkono Raila Odinga kuwa mrithi wake ni “kinyume cha kiapo kilicholishwa watu wa jamii ya Gema mnamo 1969”.
Bw Kung’u Muigai anasema waliokula kiapo hicho waliapa kuzuia babake Bw Odinga, Oginga Odinga na uzao wake kuchuka madaraka ya kuongoza Kenya.
Bw Kung’u alisema waliokula kiapo hicho wanapasa kutakaswa kabla ya kumuunga mkono Bw Odinga, la sivyo jamii ya Mlima Kenya ‘itapatwa na laana’.Alieleza kuwa uamuzi wa Rais Kenyatta kumuunga mkono Bw Odinga sio wa familia yote ya Kenyatta, mbali ni wake kama mtu binafsi.
Next article
Ruto apata pigo wandani wake wakiamua kujiunga na Jubilee
[ad_2]
Source link