Connect with us

General News

Bodi ya kampeni yatoa hakikisho kumpeleka Raila Ikulu mwaka huu – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Bodi ya kampeni yatoa hakikisho kumpeleka Raila Ikulu mwaka huu – Taifa Leo

Bodi ya kampeni yatoa hakikisho kumpeleka Raila Ikulu mwaka huu

Na JAMES MURIMI

MWENYEKITI wa bodi ya kufanya kampeni ya Urais kwa Kinara wa ODM Raila Odinga, Ndiritu Muriithi ameahidi kuweka juhudi na kuhakikisha kwamba Bw Odinga ameshinda katika uchaguzi Mkuu wa Agosti, 9.

Akizungumza na wanahabari jana katika mji wa Nanyuki, Bw Muriithi alisema ana imani kwamba timu hiyo ya wanachama 11 itamletea ushindi Bw Odinga dhidi ya mpinzani wake mkuu, Naibu Rais, William Ruto.

“Sina shaka hata kidogo kwamba Bw Odinga atakuwa Rais wa tano wa Jamhuri ya Kenya. Dalili zote zinaonyesha kuwa yeye ndiye kiongozi anayestahili,” akasema Bw Muriithi.

Gavana huyo wa Laikipia alisema kuwa timu ya ngazi ya juu ya kuimarisha umaarufu wa Bw Odinga na kuwashawishi wananchi wanaotoka mashinani itaundwa hivi karibuni.

Bw Muriithi alisema Bw Odinga amefanya majaribio mengi ya kunyakua nyadhifa za juu zaidi za uchaguzi nchini, akiongeza kuwa anastahili kupewa nafasi ya kuongoza na kuunganisha Wakenya.

“Kusema ukweli, viongozi wengi wakuu hata kwenye makampuni si lazima wafanikiwe katika jaribio la kwanza. Hata hivyo, Bw Odinga amewania kiti cha urais mara nyingi. Mwaka huu, nina imani kuwa yeye ndiye atakayechaguliwa kuwa rais wa Jamhuri ya Kenya.”

Alisema kuwa watu wa Mlima Kenya tayari wameonyesha dalili za kumuunga mkono Bw Odinga na hata kuunga azimio lake la kuwaleta Wakenya pamoja.

Kadhalika, alisema Bw Odinga amejitolea kwa miaka mingi kuikomboa nchi kutoka kwa udikteta katika miaka ya 1990, akiongeza kuwa ulikuwa wakati mwafaka kwa Wakenya kumuunga mkono na kumchagua.

“Uhuru tunaofurahia sasa haukutokea tu. Ni kwa sababu Bw Odinga na viongozi wengine waliojitolea mhanga na kuupigania uhuru wa nchi. Unachoweza kuchukulia kuwa cha kawaida sasa, hakikuwepo wakati huo.”