[ad_1]
AFCON: Cameroon kukutana na Gambia kwenye robo-fainali baada ya kung’oa Comoros
Na MASHIRIKA
WENYEJI Cameroon sasa watakutana na Gambia katika robo-fainali ya Kombe la Afrika (AFCON) baada ya kuwapokeza Comoros kichapo cha 2-1 mnamo Jumatatu usiku ugani Olembe, Yaounde.
Hata hivyo, ladha ya ushindi huo wa Cameroon iliyeyushwa na vifo vya watu sita na mamia kuumia kutokana na ajali nje ya uwanja. Idadi kubwa ya watu walijitokeza kutazama mchuano huo na wengi wao walishuhudiwa wakisukumana ili kupata fursa ya kuingia uwanjani na hivyo kusababisha ajali hiyo.
Uga wa Olembe almaarufu Paul Biya, una uwezo wa kubeba mashabiki 60,000. Lakini kwa sababu ya kanuni zinazodhibiti msambao wa virusi vya corona, ugani huo haukustahili kubeba zaidi ya asilimia 80 ya mashabiki.
Licha ya tukio hilo la kufa na kuumia kwa mashabiki nje ya uwanja, mechi iliendelea. Mabao kutoka kwa Karl Toko Ekambi na Vincent Aboubakar yalivunia Indomitable Lions wa Cameroon ushindi wa 2-1 baada ya Nadjim Abdou wa Gambia kuonyeshwa kadi nyekundu katika dakika ya saba.
Hata hivyo, Comoros walisalia imara na kujituma maradufu kabla ya kufungiwa bao la kufuta machozi na Youssouf M’Changama katika dakika ya 81. Chaker Alhadhur ambaye kwa kawaida ni beki wa kushoto, alijituma ipasavyo katikati ya michuma baada ya kuwajibishwa kama kipa.
Mbali na kukosa kocha, Gambia hawakuwa na wachezaji 12 tegemeo wa kikosi cha kwanza baada ya kupatikana na virusi vya corona.
TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO
[ad_2]
Source link