Connect with us

General News

Chalobah sasa kuchezea Chelsea hadi 2026 – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Chalobah sasa kuchezea Chelsea hadi 2026

Chalobah sasa kuchezea Chelsea hadi 2026

Na MASHIRIKA

BEKI wa Chelsea, Trevoh Chalobah ametia saini kandarasi mpya ya miaka minne na nusu uwanjani Stamford Bridge.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 22 ameridhisha zaidi kambini mwa Chelsea msimu huu huku akiwajibishwa na kocha Thomas Tuchel mara 10 katika mapambano yote kufikia sasa.

“Imekuwa ndoto yangu kutia saini mkataba wa muda mrefu kambini mwa kikosi ambacho kimenipokeza malezi ya soka kwa kipindi kirefu kilichopita,” akasema Chalobah kuhusu mkataba huo unaotarajiwa kukatika rasmi mnamo 2026.

Katika mchuano wake wa kwanza ndani ya jezi za Chelsea katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL), Chalobah alifunga bao kwa ustadi mkubwa dhidi ya Crystal Palace katika mechi ya kwanza ya msimu huu wa 2021-22.

Kocha aliyemlea pakubwa kitaaluma ni Antonio Conte kabla ya Chelsea kumtuma kambini mwa Ipswich, Huddersfield na Lorient kwa mkopo.

Tangu awajibishwe katika kikosi cha watu wazima ugani Stamford Bridge, Chalobah ambaye ni raia wa Sierra Leone amechezeshwa na Chelsea mara tano katika kampeni za EPL.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO