Connect with us

General News

Chama cha madaktari nchini chapinga usimamizi wa KDF KEMSA – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Chama cha madaktari nchini chapinga usimamizi wa KDF KEMSA – Taifa Leo

Chama cha madaktari nchini chapinga usimamizi wa KDF KEMSA

Na RICHARD MUNGUTI

CHAMA cha madaktari nchini (KMPDU) kimeishtaki serikali kupinga usimamizi wa mamlaka ya dawa (KEMSA) kutwaliwa na idara Jeshi (KDF).

Hatua ya Serikali kupeleka maafisa wa KDF kusimamia KEMSA kulitokana na kashfa ya Sh8bilioni ya usambazaji wa vifaa vya kupambana na gonjwa la Covid-19. Na wakati huo huo KMPDU kimeomba mahakama ya masuala ya ajira (ELRC) ifutilie mbali hatua ya kuwafuta kazi wafanyazi wapatao 910 wa KEMSA.

Wafanyakazi hao walipewa arifa za kuwatimua kazini mnamo Novemba 4, 2021. Kupitia kwa wakili Henry Kurauka KMPDU kimesema serikali haikufanya mashauari na washika dau kabla ya kuamua kupeleka maafisa wa KDF na wale wa shirika la vijana kwa huduma ya kitaifa (NYS) kuthibiti shughuli KEMSA.

Bw Kurauka ameomba mahakama iratibishe kesi hiyo kuwa ya dharura kwa vile wafanyakazi wa KEMSA wamepewa likizo ya lazima. KMPDU kimeshtaki KEMSA, Waziri wa Afya Mutahi Kagwe na Waziri wa Leba Simon Chelungui na Mwanasheria mkuu Bw Paul Kariuki Kihara.

Katika kesi hiyo, KMPDU kilicho na wanachama zaidi ya 10,000 kinasema hatua ya kuwatimua kazi wafanyakazi wa KEMSA kwa madai hawamo miongoni mwa wanaotoa huduma za matibabu hayana msingi wowote kisheria.

“Kuwapeleka maafisa wa KDP na NYS kusimamia KEMSA kunakiuka Kifungu nambari 24 (5)(d) cha katiba kinachoeleza bayana jukumu la maafisa wa kijeshi ni kulinda nchi hii dhidi ya uvamizi na yanaweza tu kupelekwa kusaidia idara nyingine za serikali kunapotokea dharura,” asema Bw Kurauka katika ushahidi aliowasilisha kortini.

Bw Kurauka anasema hakuna suala la dharura linalokumba Kemsa na kupeleka maafisa wa KDF na NYS ni kukaidi sheria. KMPDU kimesema wafanyakazi kazi wa Kemsa walielezwa kwamba mamlaka hiyo inakumbwa na uhaba wa pesa kabla ya kupewa likizo ya lazima na wengine wachache kuelezwa wafanye kazi kutoka nyumbani.