Connect with us

General News

Changamoto tele Mukuru hazikuzima bidii yao shuleni – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Changamoto tele Mukuru hazikuzima bidii yao shuleni – Taifa Leo

KCPE 2021: Changamoto tele Mukuru hazikuzima bidii yao shuleni

NA SAMMY KIMATU

WANAFUNZI watano katika mitaa ya mabanda ya Mukuru walikiuka hali ngumu ya mazingira yao na kila mmoja kuzoa alama zaidi ya 400 kwenye Mtihani wa Kitaifa wa Darasa la Nane (KCPE 2021).

Akiwapongeza na kutoa ushauri nasaha Jumanne, mkurugenzi mkuu wa Mukuru Promotion Centre (MPC), Mtawa Mary Killeen aliwataka watie bidii masomoni.

Aliambia Taifa Leo watoto hao waliathirika wakati wa mikasa ya moto mtaani.

Isitoshe, Mtawa Killeen aliongeza kwamba mafuriko mwaka 2021, janga la Covid-19, ubomozi wa nyumba kupisha ujenzi wa barabara sawia na ukosefu wa stima ni changamoto ambazo hazikuzima ari na bidii yao masomoni na hivyo wakapasi KCPE.

Watoto hao ni Fidel Okatch aliyezoa alama 400, Brian Musyoki aliyepata alama 401 na Samuel Isavwa aliyepata alama 409.

Wengine ni Gregory Ouma aliyepata alama 410 na Sharp Felix aliyezoa alama 417.

Watoto hawa watano walisomea katika shule nne za umma zilizo ndani ya mitaa mbalimbali katika maeneo ya Mukuru.

Zaidi ya hayo, shule hizo zinafadhiliwa na MPC chini ya usimamizi wa Sisters of Mercy-Kenya Chapter.

Mtawa Killeen alisema Okatch alisomea katika shule ya msingi ya St Catherine, Musyoki akiwa katika shule ya msingi ya St Bakhita huku Sharp akisomea katika shule ya msingi ya St Elizabeth.

Nao Isavwa na Ouma walikuwa pamoja katika shule ya msingi ya Mukuru.

Kuhusu maskani yao, Okatch alikuwa akitoka kila asubuhi saa kumi na moja asubuhi kutembea kutoka mtaa wa Muthurwa hadi St Bakhita South B iliyo umbali wa kilomita tano.

Musyoki ni mkazi wa mtaa wa mabanda wa Mukuru-Kamongo kwenye wadi ya Landi Mawe naye Felix ni mkazi katika mtaa wa mabanda wa Mukuru-Lunga Lunga kwenye wadi ya Viwandani, eneobunge la Makadara.

Ouma na Isavwa ni wakazi wa mtaa wa mabanda wa Mukuru-Kayaba ulioko katika kaunti ndogo ya Starehe.

Masuala mengine kuhusu watoto hawa ni kwamba walikuwa mabingwa kutoka idadi ya watahiniwa 792 kutoka kwa shule nne za msingi zinazothaminiwa na MPC.

Babake Gregory, Bw John Odhiambo, 58, aliye kadhalika baba wa watoto 10, aliambia Taifa Leo kwamba Gregory alikuwa mtoto mwerevu tangu akiwa chekechea.

“Ni mvulana mtulivu, aliye na nidhamu nzuri na anafuata nyayo za kaka yake mkubwa aliye katika Chuo Kikuu cha Kenyatta (KU). Hakuwa na baadhi ya vitabu vilivyohitajika na mara nyingi tulikuwa tukikaa gizani kwa kukosa umeme mtaani japo alifanya vizuri katika mtihani wake,” Bw Odhiambo akasema.

Kadhalika, Bw Jim Sharp, 42 ambaye ni babake Felix Sharp alisema mwanawe ni mtoto wa tatu katika familia ya watoto sita.

Sharp Felix (kulia) aliyepata alama 417 katika KCPE 2021 akiwa na babake mzazi Bw Jim Sharp. PICHA | SAMMY KIMATU

“Mwanangu alisomea katika mtaa ulio na makelele, ukosefu wa stima na changamoto za mafuriko. Hata hivyo, alitegemea usaidizi wa vitabu alivyoomba kutoka kwa marafiki tofauti,” Bw Sharp akasema.

Changamoto ya Bw Sharp ni kwamba ni kibarua katika sekta ya juakali na anakiri atakuwa na kibarua kizito kupata karo.

Kwa jumla yatafuatayo ni azimio ya wanaunzi wote watano na uraibu wao mtawalia.

Okatch angependa kusomea uhandisi wa stima na ni mchoraji shupavu.

Musyoki angependa kuwa mhandisi wa ujenzi au kuwa rubani mbali na kupenda kupaka rangi.

Isavwa huhusudu kuogelea na anatarajia kuwa mhandisi katika siku za usoni.

Ouma hupenda kabumbu huku Sharp akipendelea kusoma vitabu vya riwaya kando na kuwa mhandisi wa elektroniki na msomi wa nyota na masuala ya angani.

[email protected]