General News
Changamoto za kiafya katika viwanda vya chumvi – Taifa Leo
Published
4 years agoon
By
Taifa Leo [ad_1]

Changamoto za kiafya katika viwanda vya chumvi
Na PAULINE ONGAJI
Kwa Bi Bahati Kahindi, 45, mkazi wa eneo la Bundasaga, Kaunti ya Kilifi, maisha yamekuwa magumu.
Bi Kahindi hawezi kaa kwa jua kwa muda mrefu kwani kila anapofanya hivyo, mdomo wake unauma na kuasha kana kwamba unaungua. Hawezi tafuna chakula kwa kawaida na kila anapofikiria kupiga mswaki, yeye huingiwa na hofu.
Mwanamke huyu mama wa watoto wanane anaugua maradhi yasiyoeleweka miongoni mwa wakazi wa eneo hili. Mdomo wake umechibuka, kubadilika rangi na kuwa mwekundu. Aidha, una chembechembe za rangi ya manjano utadhani ni usaha, ufizi umebadilika na kuwa mwekundu, huku meno yake yakiwa yamemomonyoa na kusalia machonge.
“Siwezi tafuna wala kulala pasipo kukumbwa na maumivu makali na mambo huwa mabaya zaidi msimu wa jua kali ambapo siwezi enda nje,” aeleza.
Kulingana na Bi Bahati, masaibu yake yalianza takriban miaka kumi iliyopita, wakati huo akifanya kazi kama kibarua katika kiwanda cha kusafisha chumvi katika eneo hili.
“Nikiwa kazini jukumu langu lilikuwa kuvunja vipande vya chumvi, kukusanya na kutia kwenye mabeseni kabla ya kupakia kwenye trekta,” aeleza.
Tatizo lilianza kama malengelenge kwenye mdomo kabla ya ufizi kugeuka na kuwa mwekundu. “Pia nilianza kugundua kwamba meno yangu yalikuwa yameanza kumomonyoa na kulegea. Mwanzoni nilidhani kwamba yalikuwa maambukizi,” aeleza.
Ilimbidi kwenda hospitalini mara kadhaa lakini hakupata nafuu. “Nilenda katika hospitali eneo la Marereni mara kadhaa, lakini hata baada ya matibabu, sikupata nafuu na hatimaye nikachoka. Pia, singeweza kumudu hizi huduma za kila mara kwani sasa sikuwa na kazi na kupata pesa ilikuwa changamoto,” aeleza.
Hadithi ya Bi Bahati inakaribiana na ya Bi Karunda Charo ambaye pia anasema kwamba aliwahi fanya kazi katika kiwanda cha kusafisha chumvi. “Tatizo langu lilianza na maumivu ya kichwa, kisha mdomo wangu ukaanza kuasha na kuwa na malengelenge kabla ya kugeuka na kuwa vidonda vikali. Nilienda hospitalini lakini mambo hayakubadilika,” aeleza.
Zaidi ya mwongo mmoja baadaye, mdomo wa Bi Charo ungali mwekundu na una chembechembe za manjano zinazofanana na usaha. “Kuna wakati ambapo mdomo hubadilika rangi na kuwa mweupe na kuuma sana,” aeleza.
Kwa Bi Kache Sonje kutoka eneo la Kurawa Karagoni zaidi ya mwingi mmoja uliopita alilazimika kuacha kazi kiwandani baada ya kuanza kuonyesha ishara hizi. “Mdomo wangu ulianza kukauka, kuasha, kuchibuka na kuwa na vidonda. Aidha, nilianza kukumbwa na matatizo ya macho ambapo ilinibidi kuacha kazi ili kutafuta huduma za matibabu,” aeleza.
Kwa bahati nzuri Bi Sonje alipona, taswira tofauti na ile inayowakumba Bi Charon na Bi Kahindi. “Lakini bado mwili wangu umekuwa dhaifu na pindi nikijaribu kusongea mazingira ya chumvi, mdomo unaanza kuchibuka tena,” aeleza.
Bw Kahindi Mumba afisa wa afya ambaye amesimamia zahanati ya Marereni kwa zaidi ya miaka minne, anazungumzia matatizo ya kiafya ambayo yamekithiri miongoni mwa wagonjwa wanaosaka matibabu katika kituo hicho.
“Wengi wanakumbwa na matatizo ya ngozi kama vile kujikuna. Kuna baadhi yao wanaokumbwa na maradhi ya tezi ambapo tunaamini kwamba ni kutokana na matumizi ya chumvi ambayo haijasafishwa ambayo mara nyingi hukosa madini ya iodine. Kwa wale wanaokumbwa na matatizo ya ngozi tunashuku kwamba ni kutokana na kugusana na chumvi ghafi,” aongeza.
Utafiti wa awali uliofanywa na Taasisi ya Sheria na Udhibiti wa Mazingira (ILEG) ulionyesha kwamba wafanyakazi wanaohudumu katika viwanda vya kusafisha chumvi katika eneo hili walilalama kuhusu kuathirika kiafya.
Upelelezi huru wa kisayansi uliofanywa mwaka wa 2019 kwa niaba ya shirika la kutetea haki za kibinadamu la Malindi Rights Forum MRF, kuhusu dhuluma za kimazingira kwenye ukanda wa uzalishaji chumvi katika eneo la Magarini, Kaunti ya Kilifi, ulionyesha kwamba wafanyakazi katika viwanda hivyo hufanya kazi katika hali isiyoridhisha.
Mwaka wa 2006 ripoti ya tume ya kitaifa ya haki za kibinadamu KNCHR, ilionyesha kuwepo kwa matatizo tofauti ya kiafya miongoni mwa wafanyakazi wanaohudumu katika viwanda vya chumvi katika eneo hili.
Matatizo haya yalikuwa pamoja na maambukizi ya sehemu ya juu ya mfumo wa kupumua na maambukizi ya ngozi na macho, hali ambayo hasa huhusishwa na kuwa wazi kwa vumbi ya chumvi ghafi.
Kulingana na utafiti huu, mojawapo ya sababu zilizokuwa zikisababisha matatizo ya kiafya kwa wafanyakazi katika viwanda vya chumvi, ni kuwa wazi kwa kemikali kwa jina brine. Brine ni mchanganyiko mkali wa chumvi (NaCl) majini.
Aidha, wataalam waliohusishwa kwenye ripoti hii walisema kwamba mchanganyiko huu kwenye wangwa za chumvi wakati wa uvunaji chumvi ulionekana kusababisha matatizo ya ngozi kukauka, kuwa na nyufa na vidonda.
Mwaka wa 2017, KNCHR ilifanya ukaguzi zaidi endapo mapendekezo ya uchunguzi kuhusu madai ya dhuluma za kibanadamu dhidi ya kampuni za kusafisha chumvi katika eneo la Magarini, Malindi yalikuwa yametekelezwa.
Baadhi ya malengo ya ukaguzi huo yalikuwa kuchunguza mambo yaliyoafikiwa tangu uchunguzi huo wa 2006 na kutoa mapendekezo kwa minajili ya kuchukua hatua zaidi.
Bw Patrick Ochieng, wa shirika la kutetea haki za kibinadamu la Ujamaa Centre, ambalo lilikuwa likishirikiana na MRF kwenye kamati ya Rais chini ya usimamizi wa Kamishna wa eneo hilo, pamoja na Halmashauri ya Kitaifa ya Kudhibiti Mazingira NEMA, asema kwamba matokeo ya uchunguzi huo yalionyesha madai ya uharibifu wa mazingira na hali duni kazini.
Kwa upande mwingine anasema kwamba pia madai ya vitisho kutoka kwa baadhi ya viongozi wa eneo hilo, vile vile masuala ya kuharibiana sifa ni baadhi ya mambo ambayo yametia doa uhusiano baina ya viwanda hivi na jamii ya eneo hili.
Lakini kuligana na Bw Ochieng hayo yalikoomea hapo. Hawakupata majibu yoyote kutokana na matokeo ya uchunguzi. Juhudi zetu za kupata maoni kutoka kwa NEMA kuhusu hatua zilizochukuliwa baadaye, hazikufuadafu.
Lakini kulingana na Bw Kibiti Kirimi, mwenyekiti wa kitengo cha sekta ya chumvi katika Mwungano wa watengenezaji bidhaa nchini KAM, wafanyakazi wa kampuni za kuunda chumvi hufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu kila mwaka kutambua iwapo kuna madhara au majeraha ambayo yamesababishwa na mazingira ya kazini.
“Kuambatana na ripoti ya daktari, waathiriwa wanaopendekezewa kufanyiwa uchunguzi hupokea matibabu yanayofaa, na kutokana na uchunguzi wa awali hakujakuwa na rekodi yoyote ya athari zaidi za kiafya miongoni mwa wafanyakazi kutokana na shughuli za viwanda vya chumvi,” aeleza.
Mbali na hayo, asema kwamba kila mwaka kampuni hizi hufanya ukaguzi wa masuala wa kiafya ili kuchunguza shughuli na taratibu zao. “Ukaguzi huu hupeleleza iwapo mazingira ya ajira yanawaweka wafanyakazi katika hatari ya kiafya, ambapo nakala za ripoti hizi kisha huwasilishwa kwa Idara ya kudhibiti usalama wa kiafya kazini DOSH, kwa uthibitisho,” aeleza.
Lakini mbali na hayo, Bw Kirimi asema kwamba kumekuwa na tetesi kuhusiana na ubora wa vifaa vya kujilinda vinavyotumika na wafanyakazi. “Kwa kawaida DOSH huweka vigezo vya vifaa vya usalama vinavyostahili kutumika katika sekta hii. Hata hivyo, vifaa vya kujilinda kuambatana na viwango vya DOSH, havifai katika mazingira ya chumvi,” aeleza Bw Kirimi.
Jitihada za kuwasiliana na afisi za Dosh katika Kaunti ya Kilifi mara kadhaa hazikufuadafu.
Kwa upande mwingine Bw Kirimi asema, kutokana na wasiwasi huu, kitengo cha sekta ya chumvi kiliagiza mtaalam huru kufanya utafiti wa kupendekeza vifaa mwafaka vya usalama kwa wafanyakazi. “Kwa sasa tunasubiri mapendekezo ambayo tutawasilisha kwa idara husika za serikali, ili kushinikiza kuwekwa kwa viwango vinavyowlinda wafanyakazi.”
Lakini pia Bw Kirimi anawalaumu wafanyakazi wanaohudumu katika viwanda vya chumvi, huku akifichua kwamba kuna baadhi yao ambao licha ya kupewa vifaa vya kuwalinda kazini, hususia kuvitumia, na hivyo kujiweka hatarini.
Lakini hayo yakijiri, kwa Bi Bahati, Bi Charo na wengine wanaokumbwa na masaibu sawa na haya, mateso yanaendelea.
Kwa sasa Bi Charo asema kwamba hawezi tembea kwa mwendo mrefu hasa kwenye jua, mbali na kukumbwa na maumivu wakati wa kula.
Kwa upande wake Bi Bahati, amelazimika kukumbatia hali yake mpya. “Siwezi piga mswaki wala kula chakula kwa starehe. Inanibidi nile chakula baridi na kisicho na viungo vingi. Lakini hata licha ya kuzingatia haya, bado kula ni changamoto kubwa,” aeleza.
[ad_2]
Source link
Comments
You may like
South Sudan at the Brink: How Corruption Tightens Its Grip on a Rare Working Institution
Wantam Protests Hit Ugunja as CS Opiyo Wandayi Loses Support, Youths Invite DCP Led by Rigathi Gachagua
Wantam Protests Hit Ugunja as CS Opiyo Wandayi Loses Support, Youths Invite DCP Led by Rigathi Gachagua
South Sudan at the Brink: How Corruption Tightens Its Grip on a Rare Working Institution
Chepterit Comes Alive During SportyBet Kenya Gifts Motorbike to Loyal Fans
Nest Lounge Narok Under Scrutiny as KRG The Don Shooting Incident Triggers Government Silence and Maasai Community Outcry
Why the Sh323.8 Billion Kenya US Health Agreement Is Raising Data Privacy Questions
Betty Bayo’s Mother Seeks DPP Inquest Over Daughter’s Death
Ugunja Women Cry Foul After MP Appointments Snub Them Despite Campaign Support
KSh4M Serve! SportyBet Kenya Title Sponsors for Kipchumba Karori Eldoret International Volleyball Tournament
Shadrack Maritim Resurfaces in Uganda After Two-Month Disappearance
