Kifo cha muigizaji Papa Shirandula kiliwaacha wengi kwa huzuni Jumamosi Julai 18 asubuhi.
Charles Bukeko, maarufu kama Papa Shirandula, amekuwa ni muigizaji mcheshi na alipendwa sana.
Habari Nyingine: Papa Shirandula alikuwa ameambukizwa coronavirus, nduguye asema
Alikuwa ni mwenye ucheshi katika kipindi cha Shirandula.
Source: Facebook
Charles Bukeko alishinda tuzo la Kalasha mwaka wa 2010 kwa kuwa muigizaji bora zaici kwenye runinga.
Hadi kufa kwake, Bukeko alikuwa ni muigizaji kwenye kipindi hicho maarufu humu nchini na amewaacha mke na watoto watatu.
Habari Nyingine: Upepo size yake: Msanii Size 8 afichua hakuvaa chupi kabla ya kuokoka
Wakati mwingine Shiradula alifanya kazi ya kuwa mfawidhi katika kampubi mbali mbali.
Source: UGC
Bukeko alikuwa mmoja wa waandishi wa kipindi hicho ambapo alichukua nafasi yake ya kuwa mume mwenye kujikakamua mjini licha ya changamoto.
Nafasi yake na ile ya Wilbroda zilitoa picha ya mume na mke na vibwanga vyao vya ndoa kila kuchao.
Habari Nyingine: Shiro sasa: Rais Uhuru Kenyatta achangamka kuzungumza na mrembo wa Elburgon
Papa Shirandula aliigiza kama mumewe Wilibroda katika kipindi cha runinga.
Source: UGC
Muigizaji maarufu Papa Shirandula, jina kamili Charles Bukeko alikuwa amepatwa na virusi vya Covid-19.
Nduguye alisema Bukeko alikuwa amesafiri kutoka Nairobi hadi eneo la Magharibi mwa Kenya na kisha kurudi.
Habari Nyingine: Serikali kuajiri madaktari 20 kutoka Cuba kusaidia kupigana na Covid-19
Charles Bukeko wakati mwingine alipenda kuvalia kimtindo. Picha: Charles Bukeko
Source: UGC
Kando la kuwa muigizaji, Papa pia alihudumu kama mfawidhi kwenye sherehe mbali mbali na kujipatia riziki zaidi.
Wakenya walisema kifo chake ni pigo kwa nyanja ya uigizaji nchini.
Mashabiki wa Papa Shirandula waliomboleza kifo chake na kumtaja kama aliyekuwa na kipawa.
Source: UGC
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.
Subscribe to watch new videos